Sabaya na wenzake watano wafikishwa tena mahakamani leo

 


Kesi za aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (34) na walinzi wake watano, ambao wanakabiliwa na mashtaka sita na mawili ya ujambazi wa kutumia silaha zitaanza kusikilizwa leo.

Mashitaka mawili ambayo leo yanatarajiwa kuanza kusikilizwa ni ya ujambazi wa kutumia silaha ambayo mawakili wa Serikali, Tumaini Kwema, Abdallah Chavula na Tarsila Garvas walieleza kuwa upelelezi wake umekamilika.

Mashitaka hayo yatafikishwa leo mbele ya mahakimu wawili tofauti; Hakimu Mfawidhi, Martha Mahumbuga na Hakimu Mkazi Mkuu, Salome Mshasha.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post