Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 19.07.2021: Lacazette, Saul, Locatelli, Haaland, Hudson-Odoi, Coman, Jesus, Ronaldo

 

Alexander Lacazette

Arsenal inataka kumuuza mshambuliaji wake Alexandre Lacazette, 30, ili kupata fedha za usajili katika dirisha la uhamisho la msimu ujao.. (Mirror)

Inter Milan inataka kumsajili beki wa PSV Eindhoven Denzel Dumfries lakini inaweza kumnunua kwa mkopo mchezaji huyo wa Uholanzi. (Calciomercato - in Italian)

Hakujakuwa na habari yoyote mpya kuhusu uhamisho wa Saul Niguez kutoka Atletico Madrid kuelekea Barcelona na kiungo huyo wa Uhispania amekuwa akiwasiliana na klabu kadhaa huku akitarajiwa kujiunga na Liverpool au Manchester United (AS - in Spanish)

Dumfries

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Arsenal iko tayari kuilipa klabu ya Sassuolo £34m ili kumsajili kiungo wa kati wa Itali Manuel Locatelli, 23. (Fabrizio Romano via Sun)

Chelsea inajaribu kufanya kila kitu katika harakati zake za kumuwania mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, 20, ijapokuwa fursa ya kumpata mchezaji huyo kupitia mpango wa kubadilishana wachezaji iko chini . (Sky Germany - in German)

The Blues pia imempeana winga wa England Callum Hudson-Odoi, 20, kwa Bayern Munich katika mpango wa kubadilishana wachezaji ili kumsajili mchezaji wa klabu hiyo mwenye umri wa miaka 25 Kingsley Coman. (L'Equipe - in French)

Arsenal imeingia katika harakati za kumsajili beki wa Norwich na England mwenye umri wa miaka 21 Max Aarons - huku the Gunners wakiwa katika mpango wa kupata mchezaji atakayechukua mahala pake Hector Bellerin, 26. (Express)

Calum Hudson Odoi

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Everton inakaribia kumsajili winga wa England Andros Townsend, 30, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Crystal Palace na atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha mpya Rafael Benitez , Klabu hiyo pia inamsaka winga wa klabu ya Bayer Leverkusen na England Demarai Gray, 25. (Mirror)

Everton pia ni mojawapo ya klabu mbili , pamoja na wapinzani wao katika ligi ya Premia West Ham, kuwasiliana na Barcelona kuhusu makubaliano ya kumsaini beki wa Ufaransa 26, Clement Lenglet. (AS - in Spanish)

Juventus italazimika kulipa £43m ili kumpata mashambuliaji wa Brazil Gabriel Jesus kutoka Manchester City. Klabu hiyo ya Serie A imempata mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye amesalia na miaka miwili katika kandarasi yake . (Calciomercato - in Italian)

Gabriel Jesus

CHANZO CHA PICHA,BBC/TWITTER

Juventus pia inafikiria kumnunua kwa mkopo kiungo wa kati wa Argentina Leandro Paredes ,27 ili kuziba pengo la mchezaji wa Brazil Authur Melo 24 aliyejeruhiwa. (La Repubblica via Football Italia)

Barcelona ina hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Lille na Ureno Renato Sanches kwa mkopo wakiwa na fursa ya kumnunua. Mchezaji huyo mwdenye umri wa miaka 23 ana thamani ya £30m , dau ambalo Barcelona haiwezi kuafikia ili kumnunua.. (AS - in Spanish)

Renato Sancez

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Barcelona pia inaweza kumuondoa Phillippe Coutinho katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo iwapo watashindwa kumuuza kiungo mchezaji wa Brazil. Coutinho anakaribia kucheza mechi 10 ambazo zitaifanya klabu hiyo ya la Liga kuilipa Liverpool kitita cha zaidi cha £17.1m, baada ya kumsaini kutoka ligi ya Premia mwezi januari 2018.. (AS - in Spanish).

Brighton ina hamu ya kumsaini mshambuliaji wa Barcelona na Denmark Martin Braithwaite, 30, ambaye pia amehusishwa na uhamisho wa kujiunga na klabu za Wolves na West Ham. (Sport - in Spanish)

Cristiano Ronaldo alichapisha neno ''siku ya uamuzi'' katika akaunti yake ya Instagram , siku ambapo L'Equipe iliripoti kwamba uhamisho wa mshambuliaji wa Argentina Mauro Icardi, 28, kutoka Paris St-Germain kujiungana na Juventus unategemea iwapo mshambuliaji huyo wa Portugal ,36, ataondoka katika klabu ya Juve.. (AS - in Spanish)

Klabu ya Manchester United ndio klabu ya pekee inayomnyatia Kierran Trippier , lakini klabu ya Atletico Madrid inafikiria kuendelea kumzuia beki huyo wa kulia wa England 30. (AS - in Spanish)

Kiungo wa kati wa Argentina anayechezea timu ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 Luka Romero ,16, atafanyiwa vipimo vya matibabu na klabu ya Lazio siku ya Jumatatu.(Calciomercato - in Italian)

Bayern Munich inafikiria kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa Corentin Tolisso kwa dau la £17.1m mwisho wa msimu huu. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 , ambaye amehusishwa na uhamisho wa kujiunga na Napoli amesalia na mwaka mmoja na mabingwa hao wa Ujerumani. (L'Equipe via Get French Football News)

Winga wa Ufaransa Thomas Robert, mtoto wa aliyekuwa winga wa Newcastle Laurent Robert, anafanya mazoezi na klabu ya Burnley huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 akiwa na matumaini ya kujiunga na ikosi cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23.. (Sun)

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post