Upweke ni suala kuu kwa watu wazima, huku vijana wengi wakiripoti kuhisi kutengwa
Ongezeko la tatizo la upweke limeibuka baada ya marufuku ya kukaa ndani kuanza na watu kuanza kuhangaika kujitenga na wengine.
Utafiti wa mradi wa 'A Mind Cymru' ukiangalia athari za matatizo ya afya ya akili.
Mwanamke mmoja ambaye alijihisi kuwa ametengwa katika marufuku ya kutoka nyumbani anasema upweke ni tatizo kubwa sana la kiafya kuliko athari zinazotokana na uvutaji sigara au unene uliopita kiasi.
Alice Gray, mwenye miaka 29-ni mwana mawasiliano ya sayansi na mtayarishaji wa vipindi kutoka Cardiff ambaye alikuwa anahangaika na upweke wakati wa marufuku ya kutoka nje kujikinga dhidi ya corona , alisema alikuwa anapewa ushauri wa kijamii ambao ulikuwa unahitajika sana kwake".
Aliongeza kusema kuwa upweke unaonekana kuwa madai tu yanayowaathiri wazee lakini alikaa muda mrefu sana akiwa ametengwa wakati wa mlipuko wa virusi vya corona, hata alisheherekea siku yake ya kuzaliwa akiwa peke yake kwa sababu ya masharti ya watu kuwa mbalimbali.
"Upweke ni tatizo lililoenea sana ,kutokana na janga la corona lililotokea,"alisema.
"Si suala la kujitenga peke yake lakini pia suala la kuonekana kuwa la wazee wakati kuna vijana pia wanahangaika na tatizo hilo.
Akisherehekea siku ya mwisho ya kuzaliwa ya miaka yake ya ishirini , Alice aliwatamani sana maafiki zake na watu wa familia yake
Vijana wanakabiliana na tatizo la upweke mara tatu ya jinsi wazee wanavyokabiliana nalo
Baada ya kukaa miezi mingi peke yake,Bi Gray alisema yeye binafsi aliweza kunufaika na kitu katika kipindi chote cha ukiwa.
"Licha ya kuwa tatizo kubwa kisayansi lakini nadhani watu wanashusha uzito wa tatizo hilo katika ubongo wetu na afya , - kwa watu ambao wana upweke wana uwezekano mara mbili kupata matatizo ya afya ya akili na suala la upweke linachukuliwa kuwa na hatari kubwa zaidi ya uvutaji sigara au uvutaji.
"Nadhani kuwa na huduma kama za ushauri hata kwa mbali kunaweza kuwa na athari katika afya ya akili na mwili katika kiwango cha mtu au kwa ujumla.
Ushauri wa kijamii wa namna gani?
Ushauri nasaha unatoa huduma ya kusaidia mtu kutofikia katika tatizo kubwa Zaidi haswa ukiwa hautoki kliniki.
Ni jambo ambalo jumuiya flani inajipanga na kupanga au kubuni kuwa na shughuli mbalimbali kama vile klabu za bustani , kuwa na kipindi cha kucheza au kuwasiliana katika makundi.
Kabla ya janga la corona kuwa kubwa, madaktari wa chuo cha Royal walisema: "Upweke unaweza kuwa mbaya kwa wagonjwa pia na kunaweza kumfanya mgonjwa kuumwa kwa muda mrefi Zaidi.
"upweke inawaweka watu 50% kuwa kwenye hatari Zaidi ya kifo cha mapema.
"Inaweza kuwa vigumu ,kwa watu ambao wana upweke kutafuta msaada. Ndio maana tunataka ushauri wa kijamii kutumika na wale watu ambao wana utaalamu kusaidia watu ambao wana upweke au ambao wako kwenye hatari ya kufikia upweke kwa namna nzuri.
Ushauri wa masuala ya kijamii unasaidia katika kukabiliana na mambo mengi katika maisha ambayo yanaweza kukufanya usiwe na furaha au kuwa na wasiwasi.
Kuangazia masuala haya yanahitaji muda wa ziada na kukubali kuunga mkono maelekezo ambayo yanaweza kutolewa katika kusaidia kufanya shughuli mbalimbali katika jamii husika .
Ninazungumzia shughuli mbalimbali ambazo zinaweza kusaidia kupata marafiki wapya na kukufanya usiwe peke yako.
Corona na ushauri nasaha wa kijamii
Upweke wakati wa janga la Corona ulisababishwa ni marufuku ya watu kutotoka nje, watu wakilazimishwa kuwa mbali na familia, marafiki na kushindwa kukutana na marafiki wapya.
Corona ilizuia jamii kutoshirikiana kwa mengi , lakini sasa makundi yanaweza kukutana
Kwa mujibu wa Mind Cymru, ushauri nashaha wa kijamii umekuwa ukitolewa kwa wale ambao wana matatizo ya afya ya akili kwa kutumia njia ya simu au mtandao, kwa kutoa msaada wa mikakati ya kusaidia.
Marufuku hiyo ilivyopunguzwa kwa kuruhusu uwepo wa vikao vya nje katika makundi ya watu pia yameweza kuruhusu mambo mengi kuanza kufanyika tena.
"Ushauri nasaha wa kijamii ni suluhisho katika matatizo ya afya ya akili na ufadhili zaidi unahitajika ili kukabiliana na tatizo hili.