Nigeria:Wanajeshi Wanawake wana jukumu gani katika usalama wa Nigeria?

 

Wanawake wa jeshi la Ulinzi wa Kiraia wamepewa jukumu la kulinda shule za sekondari dhidi ya kuteka nyara wanafunzi

CHANZO CHA PICHA,NSCDC

Wanajeshi wanawake ni sehemu ya vikosi vya usalama vya nchini Nigeria vinavyopambana na makundi eneo la kaskazini magharibi na wanamgambo wa Boko Haram kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Wanawake wanaojitolea wamezungumzia changamoto za usalama zinazokabili Nigeria.

Mwezi Januari, wanajeshi wa kike 300 walipelekwa maeneo ya barabara kuu inayounganisha Abuja-Kaduna kusaidia operesheni za kiusalama , hasa katika mapambano dhidi ya watekaji nyara wanaodai fedha.

Inaaminika kuwa wamepelekwa uwanja wa vita kwasababu ya changamoto za kiusalama zinazokumba sehemu kadhaa za Nigeria.

Wataalamu wanaamini kuwa maafisa wa usalama wanawake wana ufanisi katika kushughulikia matatizo ya usalama hasa katika jukumu lao la kuzuia mashambulio ya kigaidi dhidi ya wanawake na kutoa ulinzi kwa shule ambazo utekaji nyara ni jambo la kawaida.

Na wataalamu wanasema wanawake wako vizuri katika kupatanisha pande mbili zilizo kwenye mgogoro.

Nigeria inaendelea kukabiliwa na changamoto za usalama katika kila sehemu ya nchi, na kusababisha serikali kutoa wito kwa raia wote kuchangia kuleta usalama.

Magavana wanaona umuhimu wa serikali kuomba msaada wa wanajeshi wa kigeni au mamluki kupigana na kundi la jihadi la Boko Haram.

Mbali na ghasia zinazotokana na shughuli za wanaotaka kujitenga kusini-mashariki, kumekuwa pia na mashambulio ya majambazi na watekaji nyara na mapigano ya kikabila na mapigano kati ya wakulima na wafugaji katika maeneo mengine.

Wakati haya yote yanatokea, wanawake na watoto ndio walio katika hatari zaidi. Kwa hivyo wanawake wana jukumu gani katika kuboresha usalama nchini Nigeria?

Wanajeshi 300 wa kike wametumwa kusaidia shughuli za usalama kwenye barabara kuu ya Abuja-Kaduna

CHANZO CHA PICHA,KADUNA STATE GOVERNMENT

Yeyote anayefuatilia habari kutoka nje ya Nigeria anajua unyanyapaa unaoambatana na barabara kuu ya Abuja-Kaduna kama matokeo ya mauaji na watu wanaotafuta kikombozi na watu wenye silaha karibu kila siku.

Mbali na hatua zingine ambazo viongozi walisema wanachukua, mwishowe waliamua kupeleka jeshi la kitaifa la kike kutenganisha njia na shughuli za wanamgambo.

Mnamo Januari 28, Gavana Nasir El-Rufai wa Jimbo la Kaduna alipokea wanajeshi wanawake 300.

Gavana huyo alipokea kundi la kwanza la askari wa kike kutoka Kikosi cha Wanawake cha Jeshi la Nigeria (NAWC) katika kituo chao cha Kakau kwenye barabara kuu.

Huko Kaduna, majambazi waliua watu 937 na waliteka nyara watu 1,972 mnamo 2020 pekee, kulingana na takwimu za serikali.

Kulinda shule dhidi ya mashambulizi na utekeji nyara dhidi ya watoto

Hapo zamani, wafanyikazi wa Ulinzi wa raia hawakuwa na bunduki, wakilinda usalama katika maeneo ya umma

CHANZO CHA PICHA,NSCDC

Kufikia sasa, mateka wakuu wamekuwa wasafiri kaskazini magharibi mwa Nigeria, ambao wamelipa mamilioni kutoroka.

Lakini tangu kutekwa nyara kwa wasichana 276 wa shule ya Chibok mnamo 2014 na Boko Haram katika Jimbo la Borno, wanamgambo kadhaa wamejiunga na safu hiyo.

Tangu 2014 wakati wa kuandaa ripoti hii, karibu wanafunzi 2,000 wametekwa nyara katika shule kaskazini mwa Nigeria.

Ya hivi karibuni ilikuwa kutekwa nyara kwa wanafunzi wa FGC kutoka Birnin Yauri katika Jimbo la Kebbi, ambapo karibu wanafunzi 60 na walimu bado wanashikiliwa mateka.

Kikosi cha Usalama na Ulinzi wa Wananchi (NSCDC) kimepeleka vikosi vyake vya usalama vya kike kulinda shule dhidi ya mashambulio ya maharamia.

Kamanda wa tume hiyo, Ahmed Audi, alisema upelekwaji huo ni sehemu ya mpango wa kuzilinda shule na Wizara ya Mambo ya Ndani na Waziri wa Mambo ya Ndani Rauf Aregbesola, ambaye alikuwa ameagizwa na kamanda kuja na mpango wa kumaliza mgogoro huo. "

Kamanda aliamuru wapewe mwezi mmoja wa mafunzo na vifaa katika majimbo yote 36 ya nchi ikiwa ni pamoja na Abuja.

Kuna mpango ulioanzishwa kuhakikisha usalama wa shule baada ya utekaji nyara wa wanafunzi wa Chibok mnamo 2014 ulioitwa "Mpango wa Shule Salama".

Mpango huo unajumuisha shule zinazozunguka kuhakikisha usalama wa wanafunzi kutoka kwenye tishio la Boko Haram Kaskazini Mashariki.

Takribani dola milioni 20 zimeahidiwa kwa mpango wa miaka mitatu unaoungwa mkono na mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa (UN) wa elimu, Gordon Brown, Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza.

Baadhi ya shule za muda zimejengwa chini ya mpango huo lakini haijulikani ikiwa shule hizo zimezungukwa katika eneo hilo, na mpango huo haujumuishi majimbo ya kaskazini magharibi.

Kukomeshwa kwa mashambulizi ya kujitoa muhanga

Utafiti uliofanywa na Kituo cha Kupambana na Ugaidi uligundua kuwa, kutoka 2011 hadi 2017, Boko Haram ilitumia washambuliaji wa kujitoa muhanga wanawake kwa takribani 244 katika mashambulio 338.

Mnamo 2018, watoto 38 kati ya 48 walitumiwa na kikundi kulenga wanawake.

Waasi wa Boko Haram waliwaua watu karibu 350,000 katika majimbo ya Borno na Yobe, kulinga na ripoti ya UN ya hivi karibuni.

Bila sheria iliyoandikwa, wanaume wa jeshi la Nigeria hawaangalii miili ya wanawake wanaotuhumiwa kwa uhalifu.

Baadhi ya wanawake na watoto wao walifukuzwa na Boko Haram kutoka mji wa Baga katika Jimbo la Borno mnamo 2013 baada ya wanamgambo kuchoma moto nyumba zao

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Hii imewahimiza wanawake wengine katika Jimbo la Borno kujiunga na vita dhidi ya Boko Haram kwa nguvu zote, kusaidia kutambua na kujaribu kushambulia wanawake kupitia mikusanyiko ya kijasusi.

Mnamo Machi 9, 2018, Mkuu wa Jeshi wakati huo, Luteni Jenerali Tukur Yusuf Buratai, aliunda Kikosi cha Wanawake cha Jeshi la Nigeria (NAWC).

Kabla ya uteuzi wake, Jenerali Buratai alikuwa Kamanda wa Kikosi Kazi cha Pamoja cha Kimataifa, (MNJTF). Haishangazi hapo ndipo alipogundua umuhimu wa kuwashirikisha wanawake moja kwa moja katika masuala ya usalama.

"Kikosi kitaangazia jukumu la wanajeshi wanawake katika usalama wa Nigeria," Buratai alisema wakati huo.

Takwimu za vifo

Serikali ya Nigeria haina njia wazi ya kuwatambua watu wanaokufa kila siku nchini - iwe kwa vurugu, ukosefu wa usalama au magonjwa.

Ndio maana wanawake wengine jasiri wamejaribu kukusanya majina ya watu kama hao chini ya vuguvugu la #Secure OurLives (linda maisha yetu)

Ilizinduliwa mnamo Aprili 2021, programu hiyo imepata watu 1,499 mpaka kufikia tarehe 22 mwezi Juni.

Wanawake hao walisema walianzisha mpango wa kutafuta waathiriwa wa mizozo.

Buky Williams ni mmoja wa viongozi wa programu hiyo na aliiambia Daily Trust: "Kila wakati tunaposikia juu ya mtu kuuawa tunahisi ilifanywa na mtu lakini tunasahau kuwa mambo yanawatokea baadhi ya familia na marafiki na jamaa.

"Tunadhani tumechukua hatua zinazohitajika kuhakikisha kuwa hawapotezi maisha yao - hatutaki mambo kama haya yaendelee, hatutaki kuendelea kupoteza wapendwa wetu. Sio kwamba hakuna suluhisho kwa tatizo, sio tu. Tunahitaji kuzingatia masuala haya. "

Mwanachama wa kundi hilo, Ayisha Osori, alisema ni jambo la kushangaza kuwa Nigeria haina taarifa yoyote juu ya idadi ya watu waliouawa katika mzozo.

'Upatanisho'

Mtaalamu wa masuala ya usalama Sadiq Garba Shehu (aliyestaafu) alisema wanawake walikuwa hodari katika upatanishi kati ya vikundi hasimu.

"Azimio la 1235 la UN linasema kuwa jukumu la wanawake katika maeneo ya vita ni muhimu sana," alisema.

Nahodha Sadiq alisema kwa kuona kuwa vikosi vya usalama vya Nigeria ni vichache, "kumtumia mwanamke kutawaruhusu wanaume hao kuhamia maeneo mengine kwa sababu za usalama".

Aisha Wakil, maarufu kama Mama Boko Haram, ni mmoja wa wanawake mashuhuri katika mzozo kati ya serikali ya Nigeria na Boko Haram.

Katika mahojiano na Channel TV mnamo 2018, Aisha alisema yeye ndiye aliyeshinikiza wanamgambo wa Boko Haram kuwaachilia zaidi ya wanafunzi 100 wa shule ya upili ya Dapchi waliotekwa nyara mnamo Februari 2018.

"Walinipigia simu na kuniambia wao ndio waliowateka nyara watoto. Niliwaambia mnakubali kuuambia ulimwengu kuwa ninyi ndio mliowateka? Wakasema ndio," alisema. "Pia niliuambia ulimwengu.

"Niliwaambia warudisheni watoto hawa, na nina matumaini hawatatumia siku 1,000. Waliniambia hawatafanya hivyo. Nilipowashinikiza walisema msiwe na wasiwasi watawarudisha."

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post