Tags
bongo habari
Ndege ya abiria yapoteza mawasiliano angani na idara ya ufuatiliaji Urusi
byben
-
0
Ndege ya Urusi iliyowabeba watu 28 imepoteza mawasiliano na idara inayofuatilia ndege angani katika rasi ya Kamchatka kusini mwa nchi hiyo.Msemaji wa idara ya uchukuzi Valentina Glazova ameliambia shirika la habari la AFP kwamba ndege hiyo aina ya An-26 ilikuwa ikisafiri kutoka mji mkuu wa rasi ya Kamchatka Petropavlovsk kuelekea mji wa bandarini Palana, wakati ilipotoweka na haikutua katika muda uliotarajiwa.Ameongeza kuwa ndege hiyo ilikuwa na jumla ya watu 28 miongoni mwao abiria 22 na wahudumu sita. Amesema shughuli ya kuitafuta ndege hiyo inaendelea.