Wauzaji wa Amazon waliouza biashara zao na kuwa mamilionea

 

A range of the products sold by firms now owned by Thrasio

CHANZO CHA PICHA,THRASIO

Maelezo ya picha,

Kampuni ya Thrasio sasa hivi ina makampuni ya bidhaa mbalimbali katika maeneo mengi

Kuwa milionea haikuwa sehemu ya mpango wangu. Michele Venton alikuwa ameondoka London na kwenda Bournemouth, akiwa makini kutaka kuachana na maisha ya kufanyakazi katika kampuni na kuamua kujaribu kuanza kuuza nguo mitandaoni.

"Kila wakati nilikuwa na wazo la kuunda magauni ya kipekee ya wanawake," anasema.

Alipata kampuni ya kumtengenezea magauni ya mtindo wa kujifunga kwa mbele na kuorodhesha bidhaa zake katika mtandao wa Amazon kwa ajili ya mauzo, ambapo alishangazwa na jinsi watu walivyovutiwa nazo.

"Mara moja nilianza kujishughulisha na hilo, - Kulikuwa na fursa kubwa huko," anasema.

Nguo, ingawa, haikuwa bidhaa rahisi kuuza mtandaoni - kulikuwa na matatizo mengi ya ukubwa, wengi walirejesha nguo walizokuwa wamenunua.

Amazon worker

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Amazon inaruhusu mtu mwingine kutumia mtandao wake wa usambazaji bidhaa kwa wateja

Lakini mama huyo wa watoto wawili, alikuwa amepitia hisia mbaya pale watoto wake walipokuwa wanaenda kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa siku chache zijazo lakini bado hajapata zawadi ya kuwapa kwenda kutoa.

Alianza kuuza zawadi za haraka haraka kwa wazazi kupitia mtandao huo wa Amazon.

Na chini ya kipindi cha miaka minne, biashara yake ilikuwa na thamani ya karibu pauni milioni 10 kwa mwaka, kote barani Ulaya na Marekani.

Lakini muda mfupi baadaye, biashara yake ikaanza kunawiri zaidi na kukua. Kutafuta mamilioni ya pauni kununua bidhaa zote alizotaka kwa kipindi kilichosalia cha mwaka ilikuwa changamoto. "Ilimhitaji mtu kuwa na mtaji wa kutosha kweli," anasema.

Mwaka 2019, alipopata ombi la kutaka kununua biashara yake yote - kwa kima cha mamilioni kadhaa - alikubali.

Amazon inaruhusu wauzaji wengine kuorodhesha bidhaa zao kwenye tovuti yao na hata kuwasilisha bidhaa hizo kwa wateja kupitia mtandao wake wa usafirishaji.

The Kiwango kikubwa cha uuzaji Amazon, kuna maanisha kwamba ikiwa watapa bidhaa na haki za uuzaji, wauzaji wadogo wadogo wanaweza kujikuta wakiuza kiwango kikubwa cha bidhaa kwa haraka.

Huku janga la corona likilazimisha wengi kufunga maduka yao, wengine wengi wameshuhudia ukuaji wa mauzo yao kiasi kwamba imekuwa vigumu kukimu mahitaji ya wateja wote.

Miaka miwili iliyopita pale Bi. Venton alipouza biashara yake, ilikuwa ni nadra sana kuuza biashara yako kwa kuwa muuzaji kupitia mtandao wa Amazon.

Mnunuaji ambaye ni mtu binafsi, alisisitiza kuwa tusiwataje au biadhaa zao kwa hofu ya kwamba atakuwa anavutia washindani au wahujumu - hivyo ndivyo mambo yalivyo katika dunia ambayo ushindani wa kibiashara mtandaoni uko juu.

Lakini kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita, kumeibuka makampuni mengine ambayo yametoa fursa kwa wajasiriamali wa Amazon kama Bi. Venton namna ya kuuza biashara zao.

Moja ya biashara inayofahamika sana Marekani kufanya hivyo ni ile ya Thrasio, ambayo ilitajwa baada ya shujaa wa Amazon, kulingana na hekaya za Kigiriki . Wananunua biashara moja hadi tatu kwa wiki, wakiwa na karibu biashara 10 Uingereza na hitaji lao linazidi kuongezeka.

Thrasio founder Josh Silberstein

CHANZO CHA PICHA,THRASIO

Maelezo ya picha,

Mwanzilishi wa kampuni ya Thrasio, Josh Silberstein amesema kuwa sasa hivi sio rahisi kwa wanaofanya biashara ya rejareja katika mtandao wa Amazon kuuza

Ikiwa ilianzishwa mwaka 2018 na kuanzia kutoka sufuri hadi kuwa na zaidi ya dola milioni 500 kama mapato yake kwa mwaka wake wa pili, kulingana na mwanzilishi wake Josh Silberstein.

"Mwaka huo [2018], ilichukua miezi saba kuuza kampuni, kulikuwa na wauzaji wengi zaidi kuliko wanunuaji. Yaani tajriba yote hiyo ilikuwa mbaya kweli kwa wauzaji," amesema.

Miaka mitatu tu baadaye, kuna kampuni 64 kote duniani zilizoanzishwa kununua biashara zilizopo Amazon. Na kwa pamoja, inakadiriwa kuwa wamefanikiwa kupata karibu dola bilioni 6 tangu Aprili 2020.

A range of the products sold by firms now owned by Thrasio

CHANZO CHA PICHA,THRASIO

Maelezo ya picha,

Kampuni ya Thrasio sasa hivi ina makampuni ya bidhaa mbalimbali katika maeneo mengi

Wauzaji wa bidhaa nyingi Amazon wanavutia wawekezaji kwasababu mara nyingi huwa na faida kubwa kulingana na washindani wao ambao sio wa mtandaoni licha ya kwamba wanauza bidhaa kidogo.

Kampuni zinazonunua biashara huwa na matumani kwamba kwa kuleta pamoja ustadi wa kitaalam na raslimali za biashara kubwa, wanaweza kusaidia biashara hizo kukua kwa haraka na kuwa na faida hata zaidi.

Mmoja wa wanunuaji ilikuwa kampuni ya Davaon, iliyoanzishwa na David Stephen ya bidhaa za kutengeneza bustani. Baada ya miaka mingi kusafiri kama muuzaji, na kutumia saa nyingi akiwa kwenye foleni, alikuwa anatafuta kazi itakayompa fursa ya kuwa karibu na familia yake.

David and Tracy Stephen

CHANZO CHA PICHA,DAVID SHEPHERD

Maelezo ya picha,

David na Tracy Stephen wanapanga kuanzisha kampuni mpya

Mke wake alimpendekezea kuuza bidhaa katika mtandao wa Amazon. Baada ya kozi ya dola 5,000, alibaini kile alichohisi kuwa biashara ya bidhaa za kutengeneza bustani bado hazipatikani kwa wingi.

Baada ya saa nyingi kutafuta kwenye tovuti ya Alibaba ya China mfanyabiashara atakayekuwa ana muuzia bidhaa hizo, alikuwa na biashara yake kwa jina Davaon, iliyokuwa na miundu ya kutengenezea bustani ya thamani ya dola 10,000.

Wakaanza kuuza bidhaa za kutengenezea bustani na kufikia mwaka 2020, yeye pamoja na mke wake walikuwa wanauza zaidi ya pauni milioni 2 kwa mwaka, wakiwa na kampuni inayowauzia bidhaa hizo kutoka Taiwan na bado hawajawahi kuonana ana kwa ana.

Lakini lengo la kurahisisha maisha lilikuwa mbali sana kufikiwa. "Ilifikia wakati ambapo tulikuwa tunafanyakazi kwa saa 12 hadi 15 kwa siku. Nilikuwa nafanya kazi hadi wikendi yaani sikuwa na pumzika.

Davaon secateurs

CHANZO CHA PICHA,DAVAON

Maelezo ya picha,

Stephens aliuza bidhaa za kutengeneza bustani

"Ikiwa mteja ataandika barua pepe wikendi, lazima ajibu. Nilikuwa nashughulikia bidhaa zinazoingia, tulikuwa tunazipakia bidhaa kwenye makasha sisi wenyewe na kuzituma Amazon. Hakukuwa na muda wa kupumzika kabisa."

Alianza kupokea ofa katika biashara yake mwaka jana. Kwanza, alifikiria kuwa ni washindani wao katika uuzaji na kuanza kutafuta taarifa zaidi.

Bwana Stephen anapanga kuanzisha biashara mpya na Bi. Venton tayari ameanzisha biashara nyengine Amazon ambayo inaangazia "bidhaa za nyumbani" - lakini hofu yake kubwa ni kuibuka kwa watu watakaokuwa wanamuiga.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post