Adhabu ya kifo ama kunyongwa mpaka kufa, imekuwa ikitekelezwa na mataifa mengi kwa muda mrefu, iliyoonekana adhabu ya kawaida kwa makosa kama unajisi, biashara ya dawa za kulevya, ufisadi na mauaji ya halaiki. Zipo nchi zilizotoa adhabu ya kunyongwa mpaka kufa kwa watu waliokuwa wanaleta upinzani na kutishia nafasi za watawala wakionekana ni kama wanatishia usalama wa nchi ama wanasaliti taifa.
Kwa sasa adhabu ya kunyongwa mpaka kufa inapingwa na watetezi wa haki za binadamu ikionekana inakwenda kinyume na haki ya binadamu ya kuishi. Mpaka sasa nchi 108 zimeondoa kabisa adhabu hiyo.
Kwa mujibu wa Shirika la kimataifa la Amnesty International watu 483 katika nchi 18 duniani walinyongwa mwaka 2020, ikiwa ni pungufu kwa asilimia 26% ukiinganisha na mwaka 2019. Pamoja na hilo unazija nchi zinazoongoza kwa kunyogwa watu duniani?
Pia Shirika hilo la Amnesty International limerekodi angalau hukumu za vifo 1,477 katika nchi 54 mwaka jana. Agalau watu 28,567 walikuwa wanasubiri kunyongwa duniani kufikia mwishoni mwa mwaka 2020
CHINA
Inaelezwa kila mwaka China inanyonga zaidi ya watu 1,000 wengi wao ni wale wenye makosa ya dawa za kulevya. Kwa mwaka jana pekee zaidi ya watu 1,000 walinyongwa kwa mwaka jana pekee nchini humo ikitajwa kuongoza duniani kutekeleza adhabu hiyo ya kunyonga. Rekodi ya Amnesty International ya watu 483 haijaijumuisha China. Ingawa hakuna ripoti rasmi kutoka kweye Mamlaka za nchi hiyo, Amnesty inabainisha China kuwa taifa lenye kutekeleza adhabu hii karibu mara mbili ya mataifa mengine. Kwa takwimu hiyo, inakadririwa watu zadi ya 10,000 wamenyongwa katika kipidi cha miaka 10 iliyopita.
MISRI
Nchi ya Misri inatajwa kuongoza Afrika, ikiwa miongoni mwa nchi tano za juu duniani zinazotekeleza adhabu ya kifo kwa kiwango cha juu. Kwa mfano katika kipindi cha kuanzia mwaka 2013 mpaka 2020, idadi ya watu walionyongwa nchini Misri inakadiriwa kuvika 150, ambayo ni mara kenda zaidi ya ile ya mwaka 2013 walipongonywa watu 32 tu.
Ingawa katika kipidi cha miaka miwili kati ya 2018 na 2019 Misri ilitoa hukumu ya kifo kwa watuhumiwa1,152 wa makosa mbalimbali lakini iliwanyonga watu 75 pekee. Huku wengine maelfu wakisubiri kutekelezwa kwa adhabu hiyo.
IRAQ
Kati ya mwaka 2011 mpaka 2019 Iraq imenyonga watu zaidi ya 800, wakati mwaka 2020 pekee chi hiyo imenyonga watu 45, ingawa ni pungufu ukilinganisha na mwaka 2019 iliponyonga watu karibu 100, bado idadi hiyo inatajwa kuwa kubwa zaidi unapozungumzia nchi zinazonyonga watu wengi. Kama ilivyo kwa Saudi Arabia, kunyogwa kwa kamba na kwa risasi ni njia inazotumia zaidi.
SAUDI ARABIA
Takribani watu 1,121 walinyongwa nchini Saudi Arabia katika kipindi cha kati ya waka 2011 mpaka 2019 kwa mujibu wa Shirika la takwimu la masuala ya adhabu za vifo (DPIC). Saudi Arabia, Iran na Iraq ni mataifa matatu yeye asilimia zaidi ya 80% ya vifo vitokanavyo na adhabu ya kunyongwa, ukiacha China. Nchi hii inatekeleza adhabu ya kifo kwa aina tatu kubwa, ukiacha kunyongwa ambayo ndiyo ya kawaida na iliyozoeleka zaidi, sindano na kupingwa risasi ni njia nyingine maarufu za kutekeleza adhabu ya kifo.
Hata hivyo nchi hii imefanikiwa kupuguza idadi ya watu inayowanyonga kwa sasa kwa mwaka, ikipunguza kwa asilimia 84% kutoka watu 184 mwaka 2019 hadi watu 27 mwaka 2020. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Amnesty International.
IRAN
Moja ya mataifa yanayotekeleza zaidi adhabu ya kifo ulimwenguni. Takwimu rasmi kutoka Shirika la takwimu la masuala ya adhabu za vifo (DPIC), inaonyesha kuwa nchi hiyo imenyongwa watu zaidi ya 3,700 katika kipindi cha miaka tisa kati ya 2011 mpaka 2011. Mwaka 2019 pekee zaidi ya watu watu 251 walinyogwa kwa makosa mbalimbali, ikiwa ni pungufu kwa watu watatu ukilinganisha na mwaka 2018. Lakini mwaka 2015 ilifikia idadi kubwa zaidi ya kunyonga watu 977.