Paris St-Germain ipo katika mazungumzo yaliopiga hatua ili kumsajili beki wa Uhispania Sergio Ramos kupitia uhamisho wa bila malipo baada ya kandarasi ya mechezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 kukamilika na klabu ya Real Madrid. (ESPN)
Manchester United inafikiria kumsaini mshambuliaji na wameafikia kumsajili mshambuliaji wa England na Everton Dominic Calvert-Lewin, 24, kama mchezaji wanayemtaka . (Sun)
Kiungo wa kati wa England Declan Rice 22, amekataa ofa mbili za kandarasi kutoka West Ham na anataka kuelezewa kuhusu ombi lolote kutoka kwa Chelsea , Manchester united na Manchester City (Guardian)
Mkufunzi mpya wa klabu ya Tottenham Hotspur Nuno Espirito Santo ameambiwa nahodha Harry Kane ,27, hatauzwa bila ya baraka zake , ijapokuwa mshambuliaji huyo wa England anatarajiwa kuelezea mpango wake wa kuondoka katika klabu hiyo.. (Telegraph - subscription required)
Everton inatumai kuishinda Arsenal katika usajili wa beki wa Brighton Ben White, 23, huku maombi mawili ya The Gunners yakiwa tayari yamekataliwa na beki huyo wa kati wa England. (Mail)
Barcelona inatumai kukamilisha mauzo ya beki wa Uhispania Junior firpo , 24, kwa leeds United katika siku chache zijazo na pia inapanga kumuuza kwa mkopo Miralem Pjanic , huku Tottenham na Juventus zikiwa na hamu ya kumsajili mchezaji huyo wa Bosnia na Herzegovina mwenye umri wa miaka 31. (Sport)
Liverpool inamchunguza kiungo wa kati wa Brighton na Mali Yves Bissouma mbali na mchezaji wa Ajax na Uholanzi Ryan Gravenberch, 19, huku wakitaka kuziba pengo lililowachwa wazi na Georginio Wijnaldum, ambaye alijiunga na PSG mapema wakati wa dirisha la uhamisho. (Liverpool Echo)
Tottenham inatarajiwa kushindana na Everton katika jaribio la kumsaini beki wa England Conor Coady kutoka Wolves.. (Football Insider)
Spurs pia imeipatia Bologna Yuro milioni 15 pamoja na gharama nyengine kwa beki wa Japan Takehiro Tomiyasu, 22, ambaye amevutia hamu kutoka kwa Man United na Atalanta. (Athletic)
Arsenal inafikiria kumuuza Willian , 32, msimu huu lakini mahitaji ya winga huyo wa Brazil hayawavutii wanaomtaka mchezaji huyo.. (Football London)
Leeds imefungua mazungumzo na Cagliari kuhusu makubaliano ya dau la Yuro milioni 30 kwa kiungo wa kati wa Uruguay Nahitan Nandez, 25. (Calciomercato - in Italian)
Real Madrid imeingia katika mbio za kumsaini beki wa Portugal Diogo Dalot kutoka Manchester United. AC Milan ipo katika mazungumzo kuhusu makubaliano ya kudumu kumsaini mchezaji mwenye umri wa miaka 22 , ambaye alikuwa na kandarasi ya mkopo na klabu hiyo ya Itali msimu uliopita. (Calciomercato - in Italian)
Aliyekuwa beki wa England Ryan Betrand , 31, amekubali kandarasi ya miaka miwili na Leicester City baada ya kuondoka Southampton wakati kandarasi yake ilipokamilika.. (Sky Sports)
Nahodha wa klabu ya Barnsley Alex Mowatt, 26, anatarajiwa kukutana na aliyekuwa mkufunzi wa zamani Tykes boss Valerien Ismael katika klabu ya West Bromwich Albion baada ya kiungo huyo wa kati kukataa kandarasi mpya. (Mirror)