Kuna hofu barani ulaya kuhusu matumizi ya teknolojia ya 3D Printing kutengeza silaha hatari na sasa sio bastola tu bali makundi ya itikadi kali za mirengo ya kulia yanayoeneza ubaguzi sasa yameanza kutengeza hadi bunduki hatari kama AK 47 na AR15.
Watu kadhaa wamekuwa wakikamatwa kote Ulaya kwa kupatikana na hatia ya kujitengezea bunduki kutumia teknolojia hiyo .
Watalaamu wanasema unachohitaji ni vifaa vya kutengeza bunduki vya gharama ya dola 50 pamoja na kupakua mtandaoni mfumo wa 3D unaokupa mwongozo jinsi ya kuzitengeza silaha hizo .
Stephan Balliet aliyehukumiwa maisha jela kwa kuwaua watu wawili ‘akifanya’ majaribio ya bunduki aliounda mwaka wa 2019 ameonekana kuwavutia watu wengi wenye misimamo mikali ya ubaguzi wa rangi tangu kesi yake ilipoangaziwa .
Ana itikadi za Kinazi ambazo zilimfanya kuwaonyesha wafuasi wake jinsi ya kuzitengeza bunduki kutumia vifaa vya palastiki na mwongozo wa 3D .
wakati akitekeleza mauaji yake hayo aliyapeperusha moja kwa moja mtandaoni .
Bunduki ya kwanza duniani kutengezwa na teknolojia ya 3D iliundwa mwaka wa 2013 na Cody Wilson, mwanaharakati wa haki za kumiliki bunduki mwenye umri wa miaka 25 huko Marekani .
Nchini Uingereza mwaka wa 2019 mshukiwa Tendai Muswere mwenye umri wa miaka 26 alishtakiwa kwa hatia ya kutengeza bastola kutumia teknolojia hiyo .Tendai kutoka katikati mwa London aliwaambia polisi wakati huo kwamba alikuwa akiitengeza bastola hiyo kwa ajili ya mradi wake wa shuleni .
Nchi nyingi za Ulaya zimekuwa zikisajili visa vingi vya kukamatwa kwa watu wanaomiliki bunduki zilizotengezwa na teknlojia hiyo ya 3D bila kuwa na leseni ya kumiliki silaha. Vifaa vinavyotengezwa na teknolojia hiyo vinaunganishwa na kuwa bunduki hatari