Taarifa iliotolewa na Barcelona kabla ya saa mbili usiku siku ya Alhamisi iliushangaza ulimwengu wa soka..
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 na raia wa Argentina , ambaye amekuwa mchezaji huru tangu Julai mosi alitarajiwa kuongeza kandarasi yake ya miaka 21 katika uwanja wa Nou Camp.
Barca ilisema kwamba kandarasi hiyo ilitarajiwa kutiwa saini siku ya Alhamisi , lakini uhaba wa fedha katika ligi hiyo ya Uhispania ulikatiza mpango huo.
Hivyobasi tunauliza je huu ndio mwisho wa Messi katika klabu ya Barca , ama kuna hakikisho la mwisho?
Kwanini makubaliano ya mkataba mpya yalianguka?
Mapema mwezi huu , mwandishi wa kandanda katika gazeti moja la Uhispania Guillem Balague alifichua kwamba Messi aliafikiana makubaliano hadi 2026 ambayo yalihusisha kupunguza mshahara wake hadi nusu .
Lakini Barca ilihitajika kuwauza wachezaji ili kufadhili makubaliano hayo ambayo yangesababisha kupunguzwa kwa mshahara wa Messi kwa Yuro milioni 200 ili kuafikia masharti ya fair Play ya ligi ya La liga- na wameshindwa kuafikia hilo.
Antoine Griezmann , Ousmane Dembele na Phillip Coutinho bado wapo katika klabu hiyo hawajauzwa .
Akizungumza na BBC ,Ballague alisema: Barca ililazimika kutafuta njia nzuri kumlipa Messi mshahara wake , na marupurupu na kila mara niliwauliza mutafanikiwa vipi kuafikia hilo iwapo hamuwezi kusajili wachezaji wapya muliowasaini bila malipo? Jibu lao lilikuwa 'tuamini tu'.
"Ujumbe kutoka kwa wawakilishi wa Messi ulikuwa kuwa na subra'',.
Rais mpya wa Barcelona Laporta alikuwa na matumaini .Hakuna hata wakati mmoja ilionekana kusema kwamba 'haiwezekani kumzuia Messi kuondoka'.
Hivi sasa imethibitisha kwamba uwezekano wa uchumi wa klabu iyo kumpatia mkataba mpya haupo.
Lakini sidhani kwamba huo ndio mwisho wa habari hiyo.
''Hali ya kifedha ya klabu hii ipo vibaya sana'' , alisema mtangazaji wa Redio mjini Catalunya Ernest Macia.
Aliambia idhaa ya BBC: watu wengi wanaendelea kufikiria , je Maisha yatakuwaje baada ya Messi kwasababu hakuna mtu alifikiria kuhusu siku hizi tatu.
"Ukweli ni kwamba , tulisikia sauti katika klabu , hata rais Joan laporta kwamba Messi atasalia. Tayari kulikuwa na kandarasi kutiwa saini.
"Katika taarifa inaonekana kwamba Barcelona na Messi walikubaliana . Badala yake inaonekana kwamba uwezo wa kifedha wa klabu hiyo , masharti ya La liga , yalikuwa hayaafikii masharti ya Fair Play FFP
Je kuna makabiliana ya kiuwezo Barcelona?
Licha ya matukeo yote hayo , tangazo la Barca halimaanishi kwamba Messi anaondoka , bado sana.
Ukweli ni kwamba , badala ya kuwa taarifa ya mwisho , ni hatua hatari katika vita vya nani mwenye uwezo na ligi ya La liga, ambayo masharti yake ya mishahara yanamzuia Messi na Barcelona kumpatia nyota huyo kandarasi mpya licha ya klabu hiyo kusema kwamba wamekubaliana.
Tatizo kuu ni uwezo wa kifedha wa klabu ya Barcelona mbali na lengo lao la kutaka kubuni Ligi kuu ya Ulaya , ambayo rais wa klabu hiyo Joan laporta ameendelea na mipango hiyo akiandamana na mwenzake wa Real Madrid Florentino Perez.
Je Messi ataishia wapi?
Ni mwaka mmoja uliopita ambapo Messi alisema kwamba alitaka kukitumia kifungu cha kumruhusu kuondoka katika klabu hiyo bila malipo lakini Barca ikasema kwamba £624m zilihitajika kulipwa mwanzo.
Hivi sada hakuna masharti kama hayo. Amekuwa akihusishwa kwa muda mrefu na uhamisho wa kujiunga na aliyekuwa mkufunzi wa Barcelona Pep Guardiola katika klabu ya Manchester City.
Lakini huku City ikimsajili Jack Grealish £100m, mbali na kuhusishwa na usajili wa mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, Balague hafikirii kwamba mabingwa hao wa ligi ya Premia wana uwezo wa kifedha kumsajili nyota huyo. Hivyobasi klabu ya pekee iliosalia kumvutia Messi ni PSG.