Barcelona ikijaribu kumbakiza Lionel Messi, inaweza kuiweka klabu hiyo katika hatari kwa miaka 50 ijayo, hiyo ni kwa mujibu wa rais wa klabu hiyo, Joan Laporta.
Messi, 34, anaondoka Barcelona kwa sababu klabu hiyo imeshindwa kumpa mkataba mpya kutokana na kubanwa na kanuni za La Liga kuhusu mishahara ya wachezaji.
Inaelezwa kuwa , kulikuwa na kampuni binafsi iliyotaka kuwekeza La Liga, hatua ambayo ingewezesha usajili wa Messi, lakini wakati huo huo, ingemaanisha Barca iachane na haki za matangazo ya Televisheni.
"Siwezi kufanya uamuzi ambao utaiathiri klabu kwa miaka 50 ijayo," alisema Laporta.
"Klabu hiii ina miaka zaidi ya 100 na iko juu ya kila kitu na kila mtu akiwemo mchezaji bra duniani. Siku zote tutamshukuru kwa kila kitu alichotufanyia.
"Ili kuwa kukidhi matakwa, tunahitaji kufanya tulilofanya, au kuiweka klabu katika wakati mgumu, Hatukuweza kuendelea na hilo, na tulipaswa kufanya uamuzi, tuliofanya."
Messi, mfungaji bora wa Barcelona wa muda wote, alikubali mkataba wa miaka 5 uliopunguzwa mshahara wake- lakini ili kufanikisha usajili wake, Klabu hiyo ilipaswa kuendelea kupunguza kiwango cha matumizi ya mishahara , kitu ambacho imeshindwa.
"Leo alitaka kubaki, kwa hivyo hajafurahia hili," alisema Laporta. "Sote tulitaka abakie. Kwa Messi anatakiwa akubaliane na hali halisi. Ndio ukweli ambao hauwezi kubadilika, na anafahamu, namtakia mema popote atakapokwenda."
Laporta aliongeza kuwa hakutaka kutoa matumaini ambayo hayapo kwamba angeweza kumbakiza Messi. "Mjadala umefungwa," alisema.(BBC SPORT)
Tangazo la Barcelona kwamba mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 34, hatabakia kwenye klabu hiyo ''limefungua mlango wa uhamisho wa kushtua " katika Manchester City. (Manchester Evening News)
Uwepo wa Messi unaweza kuathiri uwezekano wowote wa uhamisho ambao Man City walikuwa wanaupanga kwa ajili ya mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 27. (Express)
Paris St-Germain wamekuwa wakihusishwa moja kwa moja na Messi, lakini jiji kuu la Ufaransa linaonekana tu kama moja ya maeneo ambayo anaweza kwenda Muargentina huyo anayesakwa na klabu nyingi . (Le Parisien - in French)
PSG wanaonekana kuwa ndio wanaopendelewa kusaini mkataba na mshindi mara sita wa Ballon d'Or kuhamia, na uwezekano wake wa kuhamia Marekani kuchezea mojawapo ya Ligi Kuu pia upo . (Mail)
Pendekezo la Romelu Lukaku la kuhamia tena Chelsea huenda likawa linakaribia kukwama kwani mwenyekili wa klabu ya Milan Steven Zhang anataka kufikiria kwa muda zaidi kabla ya kuamua iwapo anataka kumuuza mshambuliaji huyo Mbelgiji mwenye umri wa miaka 28. (Gazzetta dello Sport - in Italian)
Manchester United bado wako makini na kusaini mkataba na mlinzi wa England Kieran Trippier, lakini Atletico Madrid wanakataa kupunguza bei yao ya pauni milioni 34 ili kumtoa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30. (Sun)
Arsenal wamefanya dau la takriban dola milioni 17 kwa ajili ya mshambuliaji wa klabu ya Lazio Muargentina Joaquin Correa, 26, ambalo "linaangaliwa kuwa halitoshi" na klabu hiyo ya Roma. (Corriere dello Sport, via Sport Witness)
Southampton wameuliza kuhusu taarifa za kusaini mkataba na Tammy Abraham, 23, kutoka klabu ya Chelsea kwa mkopo huku wakianza msako wao wa kumtafuta mtu atakayechukua nafasi ya mshambuliaji mwenzake wa England Danny Ings, 29, ambaye alijiunga na Aston Villa mapema wiki hii. (Talksport)
Arsenal wanapanga kusaini mkataba na mlinda lango wa England Aaron Ramsdale na kiungo wa kati wa Norway Sander Berge kutoka klabu ya Sheffield United, lakini dau la jumla la pauni milioni 50 huenda lisitoshe katika kuwapata vijana hao wawili wenye umri wa miaka 23 kila mmoja. (Star)
Mchezaji wa safu ya kati wa klabu ya Lyon Mfaransa Houssem Aouar, 23, amesubiri kuhamia katika klabu ya Arsenal msimu huu.(Sun)
Leicester wamejitokeza katika juhudi za kumuwinda kiungo mpya wa safu ya kati- ya mlinzi wa Ufaransa wa kikosi cha vijana wenye chini ya umri wa miaka 21 Wesley Fofana, 20, kupata jeraha la mguu wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya Villarreal Jumatano . (Sky Sports)
Meneja wa Roma Jose Mourinho amaekuwa akihusishwa na taarifa za kumhamisha kiungo wa kati wa Cameroon kutoka Fulham mwenye umri wa miaka 25 Andre-Frank Zambo Anguissa, ambaye anaweza kuigarimu klabu hiyo ya Serie A takriban pauni milioni 21 . (Gazzetta dello Sport, via Sport Witness)
Brentford wanakamilisha kusaini mkataba na winga wa Congo winger Yoane Wissa mwenye umri wa miaka 24 , kutoka klabu ya Ufaransa ya Lorient. (Sky Sports)
Crystal Palace wako katika mazungumzo ya mwisho na Blackburn kuhusu mkataba kwa ajili ya mshambuliaji Muingereza Adam Armstrong mwenye umri wa miaka 24, ambaye thamani yake ni takriban pauni milioni 20. (Sky Sports)
Palace wanaongoza katika mbio za kupata sahihi ya Armstrong licha ya ofay a awali kukataliwa na Norwich City, Southampton na Watford zote wanaweka dau lao wenyewe. (Mail)