Mashambulio ya mabomu ya 1998 : Washukiwa watatu wakuu waliohusika na mashambulizi dhidi ya Kenya na Tanzania

 

fl

CHANZO CHA PICHA,AFP

Miaka 23 iliyopita mwezi kama huu tarehe saba ,mashambulizi mawili ya kigaidi yaliotekelezwa kwa wakati mmoja yaliikumba Miji ya Nairobi, Kenya na Dar Es Salaam Tanzania.

Mashambulizi hayo ya Agosti mwaka wa 1998, yalibadilisha kabisa hali ya usalama wa kanda hii na kuzitosa nchi hizo katika kampeni iliyojulikana kama 'vita vya kimataifa dhidi ya ugaidi'.

Wiki hii tunakuletea Makala maalum kuhusu mashambulizi hayo ,wahusika wakuu na matokeo ya kampeni ya vita dhidi ya ugaidi na athari zake kwa nchi za Kenya,Tanzania ,Uganda na kanda nzima. Leo tunakupakulia sura na maelezo kuhusu wanaodaiwa kuhusika na maandalizi ,kupanga na kutekeleza mashambuliAmani na utulivu katika nchi mbili kubwa za Afrika mashariki ilikatizwa ghafla tarehe saba mwezi Agosti mwaka wa 1998 wakati mashambulizi yaliyopangwa na kutekelezwa na kundi la kigaidi yalipotokea katika balozi za Marekani katika miji ya Nairobi na Dar es Salaam.

Kenya na Tanzania zikajikuta katikati ya patashika kubwa ya ghasia za makundi ya itikadi kali za kidini na yakabeba mzigo wa gharama kubwa ya maafa ikiwemo vifo na watu wengi kujeruhiwa.

Gharama hiyo bado ipo hadi sasa ambapo makovu ya walionusurika hayajawahi kupona. Mshukiwa mkuu wa upangaji wa mashambuzi hayo ni kiongozi wa Al Qaeda aliyeuawa miaka kadhaa baadaye lakini katika mtandao wake mkubwa, walikuwepo washukiwa waliowaletea Wakenya na Watanzania maafa milangoni mwaozi hayo .

Shambulizi la Kenya lilisababisha vifo vya watu 213 na zaidi ya 4,500 kujeruhiwa ilhali nchini Tanzania watu 11 waliaga dunia na 85 kujeruhiwa.

Watu 12 kati ya waliouawa walikuwa raia wa Marekani na huo ndio uliokuwa mwanzo wa Kenya kuingia katika kampeni ya vita dhidi ya ugaidi.

Kando na mshukiwa mkuu Osama bin Laden, makala hii itakufahamisha juu ya washukiwa wengine waliohusishwa na mashambulizi hayo lakini kwanza haya ni matukio punde baada ya shambulizi hilo mwezi agosti 1998 .

  • Agosti 20, 1998 - Marekani ilielekeza makombora dhidi ya watuhumiwa wa mashambulizi hayo katika nchi za Afghanistan na Sudan kulipiza kisasi kwa mashambulizi hayo ya Afrika mashariki.
  • Agosti 27, 1998 - Maafisa wa Marekani walimshtaki raia wa Yemen Mohamed Rashed Daoud al-'Owhali na mashtaka 12 ya mauaji, moja ya kula njama ya kufanya mauaji, na moja ya kula njama ya kutumia silaha za maangamizi kuhusiana na bomu la ubalozi wa Marekani nchini Kenya .
  • Agosti 28, 1998 - Maafisa wa Marekani walimshtaki Mohammed Saddiq Odeh na mashtaka 12 ya mauaji moja ya kula njama ya kufanya mauaji, na moja ya kula njama za kutumia silaha za maangamizi. Odeh anadai kuwa mashambulizi hayo yalipangwa na al Qaeda, ikiongozwa na bin Laden.
  • Septemba 1998 - Mtuhumiwa Wadih el Hage alikamatwa huko Arlington, Texas. El Hage aliwahi kufanya kazi kwa bin Laden nchini Sudan kama katibu wake kibinafsi. El Hage hapo awali anashtakiwa kwa kusema uwongo kwa polisi na baadaye kwa kula njama ya kuwaua raia wa Marekani
  • Septemba 16, 1998 - Mamdouh Mahmud Salim, anayeripotiwa kuwa mwanachama mwanzilishi wa al Qaeda, akamatwa huko Munich, Ujerumani. Baadaye anapelekwa Marekani na kushtakiwa kwa mashambulizi dhidi ya balozi za Marekani .

Kando washukiwa hao waliokamatwa muda mfupi baada ya mashambulizi hayo , washukiwa hawa watatu walitajwa kama washukiwa wakuu katika njama nzima ya mashambulizi yaliyotokea Nairobi na Dar .

Fazul Abdullah Mohammed

Fazul Abdullah Mohammed, alikuwa kiongozi wa Al Qaeda katika Afrika mashariki na mshukiwa mkuu wa mashambulizi ya Kenya na Tanzania na aliuawa mwaka wa 2011 nchini Somalia katika ufyatulianaji wa risasi katika kizuizi kimoja cha polisi mjini Mogadishu, mji mkuu wa Somalia.

fazul

"Kifo cha Fazul ni pigo kubwa kwa Al Qaeda, washirika wake wenye msimamo mkali na shughuli zake katika Afrika Mashariki," Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani wa wakati huo Hillary Rodham Clinton alisema. "

Bwana Mohammed, ambaye alikuwa mmoja wa watu wanaotafutwa sana barani Afrika na kulikuwa na zawadi ya dola milioni 5 kutoka kwa serikali ya Marekani kwa mtu ambaye angemkamata ama kutoa habari za kufanikisha kukamatwa kwake .

Wanajeshi wa Somalia walifyatua risasi kwenye gari alilokuwamo Fazul na wakajibu kwa kuwafyatulia risasi na ndipo yeye na mshukiwa mwingine walipokumbana na mauti yao.

Bwana Mohammed, alikuwa stadi wa kujificha na alifahamu lugha kadhaa, inaaminika sana kuwa alisaidia kuleta mbinu za Al Qaeda katika kanda hii - mabomu ya kujitoa muhanga, mabomu ya barabarani na kutumia vikosi vya wapiganaji wa kigeni - dhidi wapiganaji wa Kiislam nchini Somalia .

Kulingana na maafisa wa Somalia na Marekani , aliingiza vifaa vya kutengeneza mabomu, kuchangisha pesa ili kufadhili ugaidi na kuwaleta wapiganaji wa kigeni kutoka Afghanistan, Pakistan, Chechnya na hata Marekani.

Abu Anas al-Libi

Mnamo Oktoba mwaka wa 2013 ikiwa ni miaka 15 baada ya kudaiwa kusaidia al-Qaida kupanga mashambulizi ya mabomu ya 1998 kwa balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania, Abu Anas al-Libi aliegesha gari lake kwenye barabara tulivu katika mji mkuu wa Libya.

Anas al-Liby, FBI pic from 2001

CHANZO CHA PICHA,HANDOUT

Muda mfupi baadaye, wanajeshi wa kikosi maalum cha Marekani walimlazimisha kwa bunduki kuingia kwenye gari na kuondoka kwa kasi. Walimpakia kwenye meli katika Bahari ya Mediterania kabla ya kumleta New York kushtakiwa kwa mashtaka ya kusaidia kuua watu 224, pamoja na Wamarekani kadhaa, na kujeruhi zaidi ya 4,500.

Lakini al-Libi, ambaye alikana mashtaka dhidi yake, hakuweza kuishi kuona kesi yake ikianza Januari 12 mwaka wa 2015 .

Alikufa Ijumaa tarehe 2 mwezi huo katika hospitali ya New York kwa ajili ya matatizo yaliotokana na upasuaji aliokuwa amefanyiwa wa ini. Alikuwa na miaka 50.

Al-Libi, wakati mmoja alikuwa akitafutwa na FBI na zawadi ya dola milioni 5 ilikuwa kichwani mwake, alikuwa mgonjwa wa hepatitis C wakati askari walipomkamata.

Al-Libi, kumaanisha "wa Libya" kwa Kiarabu, lilikuwa jina lake jingine la kikazi . Pia alijulikana kama Nazih Abdul-Hamed al-Ruqai, na waendesha mashtaka wa Marekani mnamo 2000 walimtaja al-Libi kuwa miongoni mwa waliokuwa katika baraza ambalo liliidhinisha operesheni za kigaidi za al-Qaida, likiwemo shambulio la Sepemba 11, 2001.

Kabla ya hapo, shambulio baya zaidi la al-Qaida lilikuwa la Agosti 7, 1998, dhidi ya balozi za Marekani huko Nairobi, Kenya, na Dar es Salaam, Tanzania.

Khalid al-Fawwaz

Alikuwa Msaidizi wa Osama bin Laden na alipatikana na hatia ya kupanga mashambulizi ya al-Qaeda dhidi ya balozi za Marekani Afrika mashariki na kuwaua watu 224 . Khalid al-Fawwaz, raia wa Saudia, alihukumiwa na mahakama ya New York Februari mwaka wa 2015 baada ya siku tatu za majaji kusikiliza kesi dhidi yake.

kk

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Alihamishwa kutoka Uingereza kwenda Marekani mwaka wa 2012 na alikabiliwa na mashtaka manne.

Al-Fawwaz, wakati huo akiwa na umri wa miaka 52, alitajwa kama msemaji wa bin Laden jijini London.

Alielezwa kuwa mmoja wa wafuasi sugu na walioaminiwa na bin Laden na hata akawa mashauri wake kuhusu habari. Mojawapo ya majukumu yake yalikuwa kuhakikisha kwamba vitisho vya bin Laden dhidi ya Marekani 'vinasambazwa na kujulikana kote duniani'

Iwapo kuna sura na wahusika nyuma ya pazia zito la magaidi waliopanga, kufadhili na kutekeleza mashambuli hayo ya 1998 dhidi ya Kenya na Tanzania, washukiwa hawa watatu ,walifahamu kilichochokuwa kikipangwa kiufanyika katika nchi hizo za Afrika mashariki kabla hata ya siku ya mkasa.


Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post