Tammy Abraham aisaidia Chelsea kuilaza Arsenal uwanja wa Emirates

Arsenal ikicheza dhidi ya Chelsea

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Tammy Abraham alifunga bao la ushindi na kuisaidia Chelsea kuilaza Arsenal 2-1 katika mechi ya kirafiki iliochezwa katika uwanja wa Emirates.

Abraham aliingilia kati pasi mbovu ya Bellerin kabla ya kufunga akiwa ndani ya boksi ikiwa imesalia dakika 18.

Granit Xhaka aliisawazishia Arsenal baada ya bao lililofungwa na kai Haverts goli lililofungwa kipindi cha kwanza.

The Gunners hatahivyo ilimpoteza kiungo wa kati Thomas Partey kufuatia jeraha la kifundo cha mguu katika kipindi cha kwanza baada ya kuchezewa visivyo na Ruben Loftus Cheek.

Kikosi cha Mikel Arteta kilidhania kimesawazisha muda wa lala salama wakati shambulio la Joe Willock lilipogonga eneo la ndani la chuma cha goli na kuonekana kupita mstari wa goli, lakini teknolojia ya golini haikutumika na bao hilo halikupeanwa.

Wachezaji wa Arsenal waliosajiliwa katika dirisha la uhamisho Ben White , Albert Sambi Lokonga na Nuno tavares wote waliingia kama wachezaji wa ziada kwa mara ya kwanza kuichezea timu yao mpya.

Mchezaji wa England , aliyesajiliwa kwa dau la

£50m kutoka Brighton alianza kwa kasi akiokoa juhudi ya Hakim Ziyech mapema katika kipindi cha pili.

Zaidi ya mashabiki 20,000 walihudhuria mechi hiyo katika uwanja wa Emirates kufuatia kupunguzwa kwa masharti ya kukabiliana na virusi vya corona, ikiwa ndio idadi kubwa kuhudhuria mechi katika uwanja huo tangu mwezi Machi 2020.

Kwengineko siku ya Jumapili, magoli kutoka kwa Fabio Silva na Ruben Neves iliipatia Wolves ushindi wa 2-1 dhidi ya timu ya Coventry katika mechi ya kirafiki.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post