Shambulio la meli ya mafuta: Hali ya wasiwasi yatanda kati ya Israel na Iran

 

Waziri mkuu wa Israel Naftali Bennet

CHANZO CHA PICHA,EPA

Maelezo ya picha,

Waziri mkuu wa Israel Naftali Bennet

Waziri mkuu wa Israel amesema kwamba anafahamu 'bila shaka' Iran ilihusika katika shambulio baya la meli ya kubeba mafuta katika pwani ya Oman , madai ambayo Iran imesema 'hayana msingi'.

Wafanyakazi wawili wa meli hiyo walifariki wakati meli hiyo ya MV Marcer Street inayoendeshwa na raia wa Israel iliposhambuliwa siku ya Alhamisi.

Waziri mkuu wa Israel Naftali Bennet alionya kwamba ''tunajua jinsi ya kutuma ujumbe'', huku Tehran ikisema kwamba ''haitasita kulinda maslahi yake''.

Kumekuwa na matukio kadhaa hivi majuzi kuhusu mashambulizi ya meli za Israel na Iran.

Mashambulizi hayo tangu mwezi Machi yameonekana kama matukio ya kulipiza kisasi.

Mwandishi wa BBC , Frank Gardner anasema kwamba vita hivi ambavyo havijatangazwa na hatua ya pande zote kupinga madai ya kutekeleza mashambulio vimekuwa vikiongezeka , lakini vifo vya watu wawili katika meli ya Marcer Street vimeashiria kwamba mzozo huo unazidi kuwa mbaya.

Mlinzi mmoja wa Uingereza na mfanyakazi raia wa Romania walifariki katika meli ya Zodiac , huku mmiliki wake na Marekani wakisema kwamba walifariki kutokana na shambulio la ndege isiokuwa na rubani. Msemaji wa wizara ya kigeni nchini Iran , Saeed Khatibzadeh, aliambia waandishi wa habari kwamba Israel inafaa kusita kutoa madai yasio na msingi.

Alisema hivi kuhusu madai hayo: 'Yeyote anayepanda upepo atavuna kimbunga'.

Ebrahim Raisi

Bwana Bennet aliambia baraza lake la mawaziri siku ya jumapili kwamba ushahidi wa kijasusi ulionesha kwamba Iran ndio iliotekeleza shambulio hilo.

Aliitaka jamii ya kimataifa kuweka wazi kwamba Iran imefanya kosa baya zaidi.

Aliongezea: 'Kivyovyote vile tunajua sisi wenyewe jinsi ya kutuma ujumbe kwa Iran'.

Iran pia imeishutumu Israel kwa kushambulia vituo vyake vya kinyuklia na wanasayansi wake.

Hatua hiyo inajiri huku kukiwa na mazungumzo mjini Viena ya kujaribu kufufua makubaliano ya mpango wa kinyuklia wa 2015 ambao unaondoa vikwazo dhidi ya Iran huku nalo taifa hilo likitakiwa kupunguza mpango wake wa kinyuklia.

Mataifa ya magharibi yanaishutumu Iran kwa kujaribu kutengeneza bomu la kinyuklia , hatahivyo Iran imekana na kusisitiza kwamba mpango wake wa kinyuklia ni wa utafiti mbali na kuzalisha umeme.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post