Tetetsi za soka Ulaya Jumanne 04.10.2022

 

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Cristiano Ronaldo

Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 37, ataruhusiwa kuondoka Manchester United mwezi Januari. (Telegraph - subscription required)

Chelsea wanaaminika kumfuatilia mshambuliaji wa Arsenal na Brazil Gabriel Martinelli mwenye umri wa miaka 21. (Mail)

The Gunners wamempa mshambuliaji wa England Bukayo Saka pauni 200,000 kwa wiki, 21, ili kuongeza muda wake wa kusalia katika klabu hiyo. (Football.london)

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Bukayo Saka

Mbali na mazungumzo na RB Leipzig kuhusu kumsajili fowadi wa Ufaransa Christopher Nkunku, 24, Chelsea pia wanajadili kumsajili beki wa kati wa Croatia Josko Gvardiol, 20, kutoka klabu hiyo ya Ujerumani. (90 Min)

The Blues pia watatathmini hali ya walinda lango katika klabu hiyo miezi ijayo, huku mchezaji wa kimataifa wa Senegal Edouard Mendy, 30, akiwa bado hajasaini mkataba mpya.. (Telegraph - subscription required)

Meneja wa Manchester United Erik ten Hag ameuambia uongozi wa klabu hiyo kutompa mchezaji yeyote kandarasi mpya hadi atakapofanya uamuzi wa nani anastahili. (Telegraph - subscription required)

.
Maelezo ya picha,

Erick ten Hag

Beki wa Ufaransa William Saliba amethibitisha kuwa wawakilishi wake wamezungumza na Arsenal kuhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kusaini mkataba mpya. (90 Min)

Meneja wa Barcelona Xavi anasema "sio wakati" kumzungumzia fowadi wa Argentina Lionel Messi, 35, kurejea katika klabu hiyo na "anataka kuwachwa kwa amani" ili kufurahia muda wake huko Paris St-Germain.. (ESPN)

Aliyekuwa meneja wa Watford Rob Edwards na bosi wa muda wa Bournemouth Gary O'Neil wako katika harakati za kuchukua nafasi ya Chris Wilder aliyetimuliwa kama meneja wa Middlesbrough. (Football Insider)

.

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Maelezo ya picha,

Lionel Messi

Bournemouth, Crystal Palace na Leicester City wanamfuatilia mchezaji wa Sheffield United mwenye umri wa miaka 23 na beki wa kushoto wa Wales Rhys Norrington-Davies. (Football Insider)

 Newcastle wamekubali kuongeza mkataba wa miaka miwili na mshambuliaji wa Uingereza Callum Wilson, 30. (90min)

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post