Kwanini Ufaransa inaipatia silaha chache Ukraine?

 

.

CHANZO CHA PICHA,ARIS MESMISS

Maelezo ya picha,

Usaidizi wa kijeshi wa Ufaransa kwa Ukraine ni asulimia 2 pekee

Iwapo Ufaransa inataka kuliongoza bara Ulaya katika kujitegemea kijeshi , ni kwanini msaada wake wa kijeshi kwa taifa la Ukraine linalopigana dhidi ya Urusi ni mchache mno?

Swali hili linaulizwa na wanamikakati wa taifa hilo ambao wanamsukumua raias Emmanuel Macron kuipatia Ukraine silaha zaidi.

Tathmini ya hivi majuzi imebaini kwamba Ufaransa imeisaidia Ukraine na chini ya asilimia 2 ya silaha zake , ikiwa ni asilimia ya chini sana ikilinganishwa na asilimia 49 ya silaha kutoka kwa Marekani na asilimia 22 kutoka Poland huku Ujerumani ikitoa asilimia tisa.

Ujerumani imechapisha orodha ya silaha ambazo imetoa au itatoa kwa Ukraine . Uingereza imeseNilihofia ukweli wa takwimu, ambazo zinasema kwamba Ufaransa ipo katika nafasi ya mwisho katika orodha ya mataifa yanayosaidia Ukraine, anaelezea Francois Gaisbourg, mmoja ya wachanganuzi wa wa maswala ya ulinzi nchini Ufaransa.

Ndio maana nilienda katika kituo cha usambazaji nchini Polanda ili kubaini ni silaha ngapi hazikuahidiwa lakini zilipelekwa Ukraine.

Hatahivyo idadi ya silaha hizo ilithibitisha hofu yangu. Ufaransa ni ya mwisho katika nafasi ya tisa miongoni mwa mataifa yanayoipatia silaha Ukraine, alisema Heisbourg.

Hata hivyo, jibu rasmi la Paris kwa hili lilikuwa kama ifuatavyo: "Ndiyo, takwimu zinakatisha tamaa, lakini mambo mengine yanafanya kazi."

Maafisa wa Wizara ya Ulinzi wanasema kipimo halisi cha msaada wa kijeshi ni ubora, si wingi. Baadhi ya nchi hutoa vifaa vilivyopitwa na wakati kwa wingi. Ufaransa ilikabidhi mitambo 18 ya silaha za kujiendesha za Kaisari ambazo zinafanya kazi kwenye mstari wa mbele wa Ukraine.

Wanaongeza kuwa Ufaransa, kama nchi nyingine za Magharibi, imepunguza hifadhi yake ya kijeshi tangu kumalizika kwa Vita Baridi.

Kuna jambo moja zaidi. Mitambo ya CAESAR, ambayo Ufaransa ililipatia jeshi la Ukraine, ni robo ya silaha zote za Ufaransa. Ikiwa itatoa zaidi, itajiweka katika mazingira magumu katika maeneo muhimu ya kimkakati kama vile Sahel na eneo la Indo-Pasifiki.

"Inaweza kuonekana kama tuko nyuma ya nchi zingine, lakini Ufaransa inakusudia kutekeleza jukumu lake," Jenerali Jerome Pellistrandi, mhariri wa gazeti la Ulinzi wa Kitaifa.

Kulingana na Geisbourg, hoja hizi zina misingi. Ikiwa Ufaransa haitashiriki katika operesheni  za shughuli za kijeshi, huenda ikajipata nje ya mipango ya kisiri ya kijeshi".

"Nilipokuwa Kyiv, kila mtu alikuwa na heshima sana kwangu. Hakukuwa na hisia kwamba Waukraine walitutendea vibaya," anasema. "Lakini kwa namna fulani ilikuwa mbaya zaidi. Nilikuwa na hisia wazi kwamba tulikuwa hatufai." .

Hali ni rahisi, kulingana na Heisbur, Ukraine itawasiliana na nchi ambazo inajua zinaweza kusambaza silaha inazohitaji na Ufaransa kwa sasa si muhimu

.

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Maelezo ya picha,

Rais Zelensky na waziri wa masuala ya kigeni nchini Ufaransa Catherine Colonna

Lakini kuna hatari nyingine kwa Ufaransa. Ukosefu wake wa uwepo nchini Ukraine unadhoofisha matarajio yake katika uongozi wa ulinzi wa Ulaya.

Nchi nyingi za Ulaya Mashariki tayari zinahofia Rais Macron, ambaye wanasema alikuwa mpole sana kwa Vladimir Putin katika miezi ya mwanzo ya vita. Ujumbe uliosambaa ni kwamba Ufaransa haina mtazamo thabiti kuhusu kuisaidia Ukraine kushinda vita dhidi ya Urusi.

Mwanasayansi maarufu wa kisiasa wa Ufaransa Pierre Aroch anaamini kwamba simulizi hili si la haki na sio sababu ya usambazaji mdogo wa silaha kwa Ukraine.

Hata hivyo, anaamini kwamba Ufaransa inapaswa kuongeza mchango wake haraka iwezekanavyo ili kuzishawishi nchi za Ulaya Mashariki, kama vile Poland, kwamba "sote tuko kwenye ukurasa mmoja."

"Lengo la Ufaransa ni kujenga sekta ya ulinzi kupitia ununuzi wa pamoja wa Ulaya. Lakini kama unataka manunuzi ya pamoja, unahitaji kuonyesha kwa nchi nyingine kuwa una maono sawa ya usalama wa pamoja," anasema.

"Ili kufanya ushirikiano wa Ulaya ufanyike, lazima tuonyeshe nchi za Ulaya Mashariki kwamba ushirikiano na Ufaransa na wazo la uhuru wa kimkakati hauna hatari za kimkakati."

Arosh anatoa wito kwa Ufaransa kuipatia Ukraine vifaru 50 vya vita vya Leclerc. Na Geisbur - mifumo ya ulinzi wa anga, ambayo, kulingana na yeye, Ukraine kwa sasa inahitaji zaidi.

"Sio ukarimu tu. Pia ni ulinzi wako."ma kwamba itatuma silaha ya kwanza ya masafa marefu kwa Ukraine.


Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post