Umoja wa Afrika watangaza kuzindua chanjo milioni 400 kwa nchi wanachama

 

Umoja wa Afrika umetangaza kusambaza dozi milioni 400 za chanjo ya corona kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika na eneo la Caribbean.

Hii ni mara ya kwanza kwa nchi wanachama wa AU kununua chanjo kwa pamoja.

Nchi kadhaa barani Afrika zitapokea shehena za kwanza za chanjo ambazo zilinunuliwa na Jumuiya ya Afrika.

Shena ya kwanza wa chanjo zitakazonunuliwa pamoja itajumuisha usafirishaji wa kila mwezi wa chanjo ya Johnson & Johnson na dozi ya kwanza ya COVID-19.

Chini ya mpango huo unaoongozwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, nguvu ya ununuzi ya pamoja ya bara ilisababisha watengenezaji wa chanjo kukubali kutoa dozi milioni 400 katika miezi ijayo.

Hatua ya mwisho ya mchakato wa utengenezaji unafanywa nchini Afrika Kusini. Karibu dozi milioni sita zinapaswa kusambazwa kwa nchi wanachama mwishoni mwa Agosti.

Chanjo milioni 400 zinatosha kuchanja theluthi moja ya watu wa Afrika katika hatua ambayo itasaidia bara hilo kufikia lengo lake la kuchanja angalau asilimia 60 ya idadi ya watu.

Nchi nyingi za Kiafrika - kwa sasa zinakabiliwa na wimbi la tatu la virusi - zina viwango vya chini kabisa vya chanjo ya corona kwa sababu zilikabiliwa na changamoto ya kupata vifaa.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post