Wavuvi wa Kenya 'wavua' mabomu ziwa Victoria

 

Kundi la wavuvi wa Kenya waliokuwa wakivua samaki katika ziwa Victoria walipigwa na butwaa baada ya kuvua sanduku kubwa la chuma lililokuwa na mabomu sita badala ya samaki.

Wavuvi hao kutoka mji wa Mbita magharibi mwa Kenya waliodhani wamepata samaki mkubwa asubuhi ya Jumatatno, walikimbilia kufungua sanduku hilo lakini walipata mambomo yenye kutu.

Polisi wa Kenya'wamekuwa wakituma ujumbe katika mtandao wa Twitter kuhusiana na tukio hilo:

Wawili kati ya wavuvi hao walipiga mbizi kwenye ziwa hilo kwa kuhofia mabomu hayo huenda yakalipuka huku wenzao watatu wakati wakiongoza boti ufuoni.

Waliripoti ugunduzi huo kwa wasimamizi wa ziwa ambao waliwajulisha polisi.

Idara ya Uchunguzi wa Makosa ya Jinai nchini Kenya (DCI) ilisema wataalam wa utupaji mabomu walijulishwa mara moja na "wakakimbilia eneo la tukio na kuchukua sanduku hilo".

Mabomu hayo yalitarajiwa kufyatuliwa baadaye na wataalam.

Mnamo mwaka wa 2019 mabomu yaliyosadikiwa kutoka enzi ya ukoloni yalipatikana yamefichwa kwenye sanduku la zamani la mbao ndani ya ziwa.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post