Rais wa Ukraine amesema mtu yoyote kutoka Taifa lolote Duniani ambaye anahitaji kuisaidia Ukraine kwenye mapambano dhidi ya Urusi aende Ukraine na atapewa silaha kwa ajili ya mapambano "Itapendeza kama wanaotupa pole watakuja pia kushiriki nasi kwenye mapambano ya kivita"
Maelfu ya Raia wa Ukraine wamevuka mipaka kuingia katika Mataifa jirani katika upande wa Magharibi kutafuta usalama wakati Urusi ikishambulia mji mkuu wa Nchi hiyo pamoja na miji mingine kwa mashambulizi ya angani.
Wengi wa waliowasili katika Mataifa hayo jirani ni Wanawake, Watoto na Wazee baada ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy siku ya Alhamisi kuwapiga marufuku Wanaume wa umri wa kujiunga na Jeshi kuondoka nchini humo.
Aidha vikosi vya Urusi vimezidu kusigea karibu na mji mkuu wa Kyiv ambapo Rais wa Ukraine Volodymyr ameendelea kusisitiza kwamba watapambana mpaka mwisho.
