HATUWEKI SILAHA CHINI, TUTAPAMBANA MPAKA MWISHO - RAIS WA UKRAINE

0

 

 


 

Wakati majeshi ya Urusi yakiwa yameuzingira Mji Mkuu wa Ukraine, Kyiv yakibakiza kilometa takribani sita kufika katikati ya mji huo, Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amejirekodi kipande kifupi cha video na kueleza kwamba yeye na majeshi yake yatapambana mpaka hatua za mwisho kuilinda nchi yake dhidi ya uvamizi wa Urusi.
 
Katika video hiyo aliyojirekodi leo, Jumamosi asubuhi, Rais Zelenskyy amesema kumekuwa na taarifa nyingi za upotoshaji katika mitandao ya kijamii zinazoendelea kusambaa kwa kasi, İkiwemo taarifa kwamba amewaambia wanajeshi wake kuweka silaha chini.
 
Rais Zelenskyy amesema bado yupo jijini Kyiv na ataendelea kuyaongoza majeshi yake kupambana na uvamizi wa urusi mpaka hatua ya mwisho na kwamba watatumia silaha zote kuhakikisha wanaishinda Urusi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable