Kutoka kwenye hotuba ya Rais wa Marekani Joe Biden amesema Wanajeshi wa Marekani ambao wamepelekwa Ulaya hawatoingia Ukraine kupigana katika vita iliyoanzishwa na Urusi
"Niseme wazi hizi ni hatua za ulinzi kabisa kwa upande wetu, hatuna nia ya kupigana na Urusi"
Mwanzoni mwa mwezi huu Rais Biden aliiambia NBC News kwamba hatozingatia hali yoyote ambayo ni pamoja na kutuma Wanajeshi wa Marekani kuwahamisha Wamarekani ambao wapo Nchini Ukraine
"Hakuna, hiyo itakuwa vita ya dunia wakati Wamarekani na Urusi wakianza kupigana risasi"
Hali ya usalama mpaka sasa ni duni nchini Ukraine ambapo Wanajeshi na raia kadhaa wameripotiwa kupoteza maisha.
Kwa habari kemkem za kuhabarisha kuelimisha na kuburudisha tembelea Msasa Online kila wakati hakika hutopitwa na chochote saa 24.
