RAIS WA UKRAINE ATANGAZA AMRI WANAUME HAKUNA KUKIMBIA NCHI..

0

 

Kutokana na hali inayoendelea nchini Ukraine Rais wa taifa hilo Volodymyr Zelensky ametangaza amri ya Wanaume wa Nchi hiyo walio na umri kati ya miaka 18 hadi 60 kutokimbia Nchi na badala yake wabaki nchini humo.
Kwenye tamko lililotiwa saini na Rais huyu siku ya alhamisi amenukuliwa akisema "ili kuhakikisha ulinzi wa Serikali, kudumisha utayari wa mapigano na uhamasishaji wa Vikosi vya Wanajeshi wa Ukraine na vikosi vingine vya kijeshi, uhamasishaji mkubwa unatakiwa kufanyika pamoja na katika mji mkuu, Kyiv na miji yote mikubwa ya Ukraine"
Ifahamike kuwa mpaka hivi sasa takriban Raia 57 wamekufa na 169 kujeruhiwa tangu Urusi ilipoanzisha uvamizi ndani ya Nchi ya Ukraine, hii ni kwa mujibu wa Waziri wa Afya wa Ukraine, Viktor Lyashko.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable