Baada ya ripoti kusambaa juu ya vikosi vya Urusi vilivyoanzisha mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Ukraine, imekua ishara ya vita kubwa zaidi inayoweza kutokea barani Ulaya tangu mwaka 1945.
Muda mfupi baada ya habari kusambaa kuhusu shambulio la Urusi dhidi ya Ukraine,
waandamanaji walikusanyika nje ya Mabalozi wa Urusi na maeneo mengine muhimu katika sehemu nyingi za dunia.
Watu walipeperusha bendera za Ukraine na kuimba kauli mbiu zinazoiunga mkono Ukraine kwenye mikutano ya hadhara mchana wa leo. Wengi wa waandamanaji, ikiwa ni pamoja na kutoka Ukraine, waliinua mabango wakisema "Ukraine itapinga" na "Sema Hapana kwa Putin".
Rais wa Ukraine "Volodymyr Zelenskyy" alilinganisha uvamizi wa Urusi nchini humo na kampeni za kijeshi zilizofanywa na Ujerumani ya Wanazi wakati wa Vita vya Pili vya Dunia.
"Urusi imeishambulia Ukraine kwa njia ya woga na ya kujiua kama Ujerumani ya Nazi ilifanya wakati wa Vita vya Pili vya Dunia," alisema katika mkutano wa mtandaoni, ambapo aliwataka raia wa Ukraine "kutoka nje" na "kuandamana dhidi ya vita hivi".
Hali kwa sasa bado si Shwari na mijadala mikubwa imezidi kuibuka huku wengi wakiomba suluhu ya mzozo huu ipatikane mapema ili kuepusha vifo vya wasio na hatia.
