Mamlaka ya udhibiti wa mawasiliano nchini Urusi imeweka ZUIO la matumizi ya maneno matatu katika kuripoti kuhusu vita ya Urusi na Ukraine kwenye vyombo vya habari nchini humo na watakao kiuka watafungiwa kurusha matangazo.
-
Maneno yaliyopigwa marufuku katika kuongelea vita ya Moscow dhidi ya Ukraine kama 'Shambulio' [Assault], Uvamizi [Invasion], au Kutangaza Vita [Declaration of war].
-
Urusi inataka vita hii iripotiwe kwenye vyombo vya habari kama Operesheni ya Kijeshi na sio Vita dhidi ya raia wa Ukraine.
