Msanii Nandy ameamua kuwaweka sawa wale wote wanaodhani yeye anafanya kiki au labda kweli mahusiano yake yamevunjika hiyo ni baada ya siku za hivi karibuni kuonekana akiwa anapost vitu kama mtu aliyeumizwa katika mapenzi huku yeye akisema anafanya hivyo ili kuwakomboa wale wanaoumizwa na mapenzi halafu hawana pakusemea
Kupitia Insta Story yake Nandy ameshare ujumbe unaosomeka hivi
"Mara kiki..Mara pole mara hivi mara vile jamaani nitaongea nitasema kinachoniumiza! Msinihukumu kabla sijaongea! Me sio msanii wa kiki najiamini mziki wangu.Ila haya yote nayo yafanya ni kwaajili ya watanzania wote wanaopitia maumivu makali ya mapenzi"
"Nimepata dm nyngi nimepata sms za kawaida nyingi simu nyingi... Nyie watu wana matatizo ya maumivu wanakufa nayo moyoni TU!! Tusipo ongea sisi vioo vya jamii nani ataongea? Lazima tufunguke ili tuokoe vizazi na vizazi.Haya mapenzi yapo tu kwanini yanatuumiza ivyo"
Na mwandishi wetu
@luckynaturebway
