Adel Zrane ambaye aliwahi kuwa kocha wa viungo wa klabu ya Simba amesema kuwa yupo tayari kurudi kufanya kazi na klabu hiyo endapo uongozi utamuhitaji kwani katika maisha ya mpira wa Afrika hakuna mtu ambaye hapendi kufanya kazi Simba
Zrane amesema
"Ni kweli nimeachana na timu ya Taifa Mauritania kwa sasa sijaongea na timu yoyote japo nimekuwa na mawasiliano ya karibu na baadhi ya viongozi wa Klabu ya Simba SC.Unajua ile ni timu kubwa na ndoto ya Kocha au mchezaji yoyote ni kufanya kazi na timu kubwa hivyo hakuna asiependa kufanya kazi na Simba wakinihitaji niko tayari kurudi Tanzania”
Zrane ambaye ni kipenzi cha mashabiki wengi wa Simba amefanya kazi Simba chini ya makocha tofauti akianza na Kocha Patrick Aussems,Sven Vandenbroeck na baadae Didier Gomes Da Rosa ambaye walitimuliwa pamoja.
