Straika wa Real Madrid, Karim Benzema ameeleza kuwa uamuzi wa Kylian Mbappe kuitosa miamba hiyo ya Bernabeu na kuamua kubaki Paris Saint-Germain (PSG) na kusaini mkataba mpya si jambo baya na wala hana shida nalo kwani wao ni marafiki na watacheza pamoja timu ya taifa
Benzema amesema
“Ningependa atimize ndoto zake za kuichezea Real Madrid, kucheza pamoja. Amechagua PSG, yatupaswa kuheshimu hilo. Kwenye uamuzi wake kuna majukumu mengi. Tutafurahi tukicheza pamoja timu ya taifa. Kila mtu ana maamuzi yake. Real Madrid ni Real Madrid, sijahuzunika. Sisi ni marafiki, hilo haliwezi kuharibu uhusiano.”
