Rais wa China atasafiri kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili


Rais wa China Xi Jinping ataondoka China kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili kwa safari Asia ya Kati


Rais wa China Xi Jinping ataondoka China kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili kwa safari Asia ya Kati ambako atakutana na rais wa Russia, Vladimir Putin, ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya kusimika nafasi yake kama kiongozi wa China mwenye nguvu zaidi toka enzi za Mao Zedong.


Ziara hiyo ya kwanza toka kuanza kwa janga la Covid-19, inaonyesha kuwa na imani kwa nafasi yake ambayo inaelekea muhula wa tatu madarakani na jukumu lake kama kiongozi wa dunia ambapo kwa sasa kuna msuguano mkubwa kwa mataifa yenye nguvu duniani.


Licha ya kuwepo kwa matendo ya uchokozi wa Russia kwa mataifa ya Magharibi kutokana na vita nchini Ukraine, mgogoro wa Taiwan na kusuasua kwa uchumi wa dunia, rais Xi anatarajia kufanya ziara rasmi Kazakhstan siku ya Jumatano.


Msaidizi wa masuala ya mambo ya nje wa rais Putin, Yuri Ushakov aliwaambia wanahabari wiki iliyopita kwamba rais wa Russia anatarajia kukutana na rais Xi, lakini hatukutoa taarifa zaidi za mazungumzo yao.

 

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post