Dakika 90 za mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Yanga SC dhidi ya KMC zimemalizika kwa. ‘Wananchi’ kuibuka na ushindi wa bao 1 -0.
Bao pekee kwenye mchezo huo lilifungwa na kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ katika dakika ya 80 ya mchezo akitumia udhaifu wa mabeki wa KMC waliyoshindwa kuzuia pasi safi iliyopigwa na Stephane Aziz Ki.
Huu ni ushindi wa sita kwa Yanga dhidi ya KMC FC kwenye michezo ya Ligi Kuu, tangu watoza ushuru hawa wa Manispaa ya Kinondoni walipopanda Ligi Kuu.
Yanga kwa sasa imefikisha pointi 17 kwenye Msimamo katika michezo 7 ya Ligi Kuu waliyocheza mpaka sasa.
Tukio la kusisimua kwenye mchezo huo ni pale ilipofika dakika ya 43 ya mchezo, mashabiki na Viongozi wa Yanga waliposimama na kuwapigia makofi viongozi wetu wote pamoja na Benchi la Ufundi kwa kutufikishia mchezo wa 43 bila Kufungwa.
Kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari, Kocha Nasredinne Nabi alisema;
Je, ulikuwa mchezo wa namna gani?
“Tulijua kuwa mechi ingekuwa Ngumu kwakuwa KMC ni timu nzuri na sisi tumetoka kwenye mchezo wa Derby dhidi ya Watani wetu hivyo”
Kuna ugumu uliojitokeza ?
“Tuliwakosa baadhi ya wachezaji wetu waliyokuwa majeruhi na wengine waliyokosa utimamu wa mwili kuendelea mchezo huu”
Kwanini baadhi ya wachezaji hawajaonekana ?
“Hatukuwachezesha baadhi ya wachezaji wetu akiwemo Kibwana Shomari, Djuma Shaban na Fiston Mayele kwa sababu wana majeraha na baadhi wamepumzishwa kwa sababu tuna michezo mingine muhimu ijayo, ”
Kocha Nabi alimalizia kwa kuwashukuru mashabiki wa Yanga kwa kumpongeza kwa kumpigia makofi ilipofika dakika ya 43 ya Mchezo
Tags
michezo