Watumiaji wengi wa simu wamekuwa wakilalamika simu zao kujaa mapema na wengi wamekuwa wakisema simu zao zinajaa pasipo kuwa na vitu vingi ndani yake. hasa kwa watumiaji wa simujanja za Android (Android Smartphones) wengi wao wamekuwa wakikumbwa na hili tatizo la uhifadhi (storage) ya simu kujaa pasipo kupata majibu au ufumbuzi.
kwenye makala hii utaenda kujifunza namna gani unaweza kuifanya simu yako iwe na nafasi ya kutosha na pengine usipate tena tatizo la simu kujaa mara kwa mara.
1: CLEAR CACHE
Unapoweka (install) programu yoyote kwenye simu yako huwa inatumia “cache file” kwa ajili ya kutunza taarifa za akiba ili kukurahisishia mtumiaji pindi unapofungua programu/App husika, lakini programu zikiwa nyingi zinazotumia cache file au kuhifadhi taarifa za akiba hupelekea uhifadhi wa simu (storage) kujaa na hivyo simu itaonyesha imejaa, hizi “cache file” hazina madhara kama zikifutwa.
Unaweza kufuta cache file (clear cache) kwa mara moja kwenye programu/Apps zote au unaweza kufuta cache file kwenye programu/App mojamoja.
(a) Kufuta/Clear-cache kwa programu/Apps zote kwa pamoja
Unapoweka (install) programu yoyote kwenye simu yako huwa inatumia “cache file” kwa ajili ya kutunza taarifa za akiba ili kukurahisishia mtumiaji pindi unapofungua programu/App husika, lakini programu zikiwa nyingi zinazotumia cache file au kuhifadhi taarifa za akiba hupelekea uhifadhi wa simu (storage) kujaa na hivyo simu itaonyesha imejaa, hizi “cache file” hazina madhara kama zikifutwa.
Unaweza kufuta cache file (clear cache) kwa mara moja kwenye programu/Apps zote au unaweza kufuta cache file kwenye programu/App mojamoja.
(a) Kufuta/Clear-cache kwa programu/Apps zote kwa pamoja
Fungua Mipangilio/Settings kwenye simu >> bofya storage >> nenda mpaka ilipo cache >> futa/clear cache
(b) Kufuta/clear cache ya programu/App moja moja
Fungua Mipangilio/Settings ya simu >> Bofya kwenye Apps >> chagua App husika >> Futa/clear cache
2: UNSTALL APPS/ ONDOA PROGRAMU
Unaweza kuondoa/unstall programu ambazo umeacha kuzitumia au unaona hauna uhitaji nazo kwa wakati huo kwa kua kila programu/app inachukua nafasi katika simu ilihali haina faida kwa wakati husika. pia kuna programu ambazo hazifanyi kazi ipasavyo unaweza kuziondoa ili kuongeza nafasi (storage) kwenye simu.
3: CLEAR APP DATA
Kila ukiweka/install programu kwenye simu, programu hiyo hutengeneza uhifadhi (storage) yake yenyewe kwa ajili ya kuhifadhi taarifa zake, mfano ukitumia kivinjari/browser Kama Google Chrome au opera n.k huwa zinatunza historia ya kivinjari/browser history zako zote na kusababisha uhifadhi/storage kujaa. unaweza kufua App data ili kuongeza nafasi/storage kwenye simu husika.
Hii inapaswa kuifanya kwa uangalifu usije kufuta App data za programu zilizokuja na simu (Built in Apps) kama Google services n.k na pia programu za mitandao ya kijamii au WhatsApp maana hukufanya kuanza kuingia (log-in) upya.
Namna ya kufuta/clear App data.
Fungua Mipangilio/Settings ya simu >> nenda kwenye Applications >> kisha bofya App husika >> storage >> Futa/clear data.
Programu/Apps kama YouTube, Google chrome, Games, n.k ndiyo zinakuwa na App data file kubwa.
4: TUMIA ANTIVIRUS/ USE ANTIVIRUS
Inashauriwa kutumia antivirus kwenye kifaa chako kwa ajili ya kuchanganua/scan na kutoa wadudu/viruses pindi wanapoingia kwenye simu yako. Tunapotumia mitandao kuperuzi au kupakua/download vitu mbalimbali basi unaweza kupakua/download file lenye wadudu/viruses na baadhi ya wadudu/viruses husababisha simu kuonekana imejaa ilihali hakuna vitu vingi kwenye simu.
5. HIFADHI FILE ZAKO/ BACK UP MEDIA FILES
Hifadhi au fanya back up vitu vyako kama photos na videos kwenye Google photos ya simu yako kisha futa/delete vitu usivyovihitaji kwa wakati huo kama picha au videos ili kuweza kuongeza nafasi ya uhifadhi (storage).
Unaweza kuipa simu yako uwezo wa kuhifadhi au kufanya back up moja kwa moja (automatically).
Namna ya kuifanya simu yako ifanye back up automatic
Fungua Settings ya simu yako >>nenda kwenye kipengele cha backup & sync kisha Chagua vitu vya kufanya backup
Njia nyingine
Fungua Settings ya simu > nenda kwenye sehemu ya accounts >chagua google >bofya Sync (put it on) kisha “Sync now“
6. FUTA VITU ULIVYOPAKUA / DELETE YOUR DOWNLOADS
Kuna vitu ambavyo siyo vya muhimu kuwa navyo au kuvitumia kwa wakati huo maana ulishavipakua/download na ukavitumia. Download folder linapatikana kwenye File manager
Fungua file manager >> all files >> download folder, hapo utaona vitu ulivyopakua na kufuta vitu ambavyo siyo vya muhimu ilikuongeza uhifadhi (storage) kwenye simu yako.