Jinsi ya kutuma picha au video kupitia WhatsApp isipunguze ubora

picha WhatsApp isipunguze ubora

Watu wengi hulalamika pindi wanapotuma picha au video zao kupitia WhatsApp zinapungua ubora na wanapoweka picha au video kwenye WhatsApp status hupunguza ubora, hii imewekwa maalumu na WhatsApp kwa ajili ya kuzuia kujaza seva (servers) zao za kuhufadhia picha au video, kumbuka kwamba picha au video yenye ubora mkubwa (high quality) ina saizi kubwa ya faili kuliko picha au video yenye ubora mdogo (low quality).

Kuna mipangilio (settings) za kubadilisha kwenye simujanja yako ili kuweza kuzuia ubora wa picha kupungua pindi unapotuma picha au video kupitia WhatsApp.

1. Fungua programu ya WhatsApp nenda kwenye mipangilio/settings (bofya doti tatu pale juu kulia)

2. Nenda mpaka kwenye storage and data >photo upload quality > Chagua sehemu ya best quality

Hapo utakuwa umeruhusu kutuma picha zenye ubora wa juu kupitia WhatsApp

Kwa Watumiaji wa Simu za iPhone.

1.Fungua programu ya WhatsApp >nenda kwenye Settings > bofya storage and data >bofya kwenye  Media upload quality > chagua best quality

Mpaka hapo utakuwa umezuia kutuma picha au video zenye ubora wa chini kupitia WhatsApp.

Njia nyingine isiyopunguza ubora wa picha unaweza kutuma picha kama Document kupitia WhatsApp, Fungua programu ya WhatsApp chagua mtu unayetaka kumtumia picha, bofya kwenye sehemu ya kuambatanisha (attach) utakuta vipengele kama Contacts, Location, Audio, Galley, Camera, Document na Poll, unatakiwa kuchagua kwenye Document kisha itakupeleka sehemu ya kuchagua hilo faili ambapo utachagua picha unayotaka kutuma. ukituma hiyo picha haitopunguza ubora wake. hii ni njia rahisi ya kutuma picha yenye ubora mzuri kupitia WhatsApp.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post