Je ni mambo gani ni muhimu sana ya kuangalia wakati wa kufanya maamuzi ya kununua TV / Runinga? Leo tutakupa ushauri bora ili kuhakikisha unapata kitu ulichokuwa unakitegemea.
Kumekuwa na maswali mengi sana juu ya vitu vya kuangalia kabla ya kununua Runinga/Television (TV), mvutano mkubwa juu ya vitu kama Smart TV, Android TV, UHD, FHD, QHD, 4K, 8K n.k.
Hili andiko litakusaidia kufahamu na kufanya maamuzi sahihi pindi ununuapo Runinga/Television (TV).
1: SMART TV AU ANDROID TV.
Kuna utofauti kati ya Smart TV na Android TV na ni kitu ambacho wengi hawakitambui kwa uzuri.
- Smart Tv: Kwa jina jingine huitwa internet TV, hii ni Runinga/TV yenye uwezo wa kuunganishwa na internet na hufanya kazi kwa mfananio sana smartphone/simujanja inavyofanya kazi. Smart TV inakuja na Programu/Applications ambazo tayari zimeweka kwenye Television ( Pre installed Applications) ambazo huwezi kuzitoa kwa pia haina sehemu ambayo utapakua (download) program nyingi ukilinganisha na kama TV hizo zingekuwa na masoko ya apps ya Google PlayStore au App Store.
- Android TV: Hii ni aina ya Smart TV ambayo inatumia programu endeshi ya Android (Android operating system), hii inakuja na sehemu unayoweza kupakua/download program zingine unazotaka kutoka kwenye soko lenye apps nyingi (kama PlayStore).
Faida moja ya Smart TV ukilinganisha na Android TV ni bora katika uharaka wa kuchakata taarifa, hasara yake ni haina sehemu ya kupakua Program zingine kama ilivyo Android TV. SmartTV isiyo kwenye mfumo wa Android TV inakuwa nyepesi zaidi kiutendaji kwani programu endeshi yake ni nyepesi sana – ikiwa na uwezo wa kutumia zile apps chache tuu.
2. Ung’avu wa picha/Resolution (HD, FHD, 4KUHD, 8KUHD)
Hizi zote zinamanisha viwango vya un’gavu wa picha au video kwenye runinga/TV yako na kadri Resolution inavyokua kubwa ndio TV inakua na uwezo mzuri wa kuonyesha picha zenye ubora zaidi na bei yake pia inakua kubwa zaidi.
Kwa wale wanaopenda kuangalia movies au kucheza Games ni vizuri ukachagua runinga/TV yenye ung’avu/resolution mzuri wa picha.
3. WIRELESS CONNECTIVITY.
Hiki ni kupengele kizuri sana cha kuangalia pindi unapotaka kununua runinga/TV, Jaribu kusoma kwenye box kama kuna vipengele/features kama Wi-Fi, Bluetooth, mirroring hizi zitakusaidia kuunganisha Runinga/TV yako na vitu kama Simu, Computer, airpods na vifaa vingine kwa njia ya Bluetooth au Internet.
4. CONNECTION NA PORTS/MATUNDU.
Angalia matundu ya yanayoweza kuunganisha vifaa vingine kwenye runinga/TV yako ili usiwe na haja ya kuchomoa chomoa nyaya unapotaka kuunganisha vifaa vingine.
5. Chapa (Brand).
Kila chapa/brand zinakua na vipengele/features tofauti tofauti kujitofautisha na chapa zingine. Kuna chapa/brands nyingi kama LG, Samsung, Sony, TCL, Hisense, Star X, Bruhm n.k.
Uchaguzi wa chapa/Brand ni wa mteja mwenyewe kulingana na bei pamoja na Features/vipengele alivyovutiwa navyo kwenye Runinga/TV husika.
7. Ukubwa wa Runinga/TV size (“inch)
Size nyingi za runinga kwa chapa/brands tofauti tofauti ni inch 32, 40, 43, 49, 50, 55, 65 kufanya maamuzi ya size ipi uchukue ni kupima umbali wa eneo itakapo wekwa runinga/TV yako na eneo ambapo mtazamaji atakaa.
Mfano umbali wa futi 4-6 nunua runinga inch 32/40, futi 5-8 unaweza nunua inch 40/43 na kuendelea.
Runinga ikiwa nzuri utapenda kuitumia kulingana na ubora au ung’avu wa picha na video, na jinsi unavyoweza kuingunisha na vifaa vingine kama simu n.k, uchaguzi wa Runinga pia huendana na matumizi ya mhusika.