Kiongozi wa upinzani Kenya adai jaribio la 'mauaji' dhidi yake

 


Waziri mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga alidai kuwa gari lake lilipigwa risasi saba siku ya Alhamisi wakati wa maandamano ya kuipinga serikali na kusema lilikuwa ''jaribio la kumuua''.

Katika kikao na wanahabari, Bw Odinga alisema polisi walilenga gari lake na la viongozi wengine wa upinzani wakati wa maandamano katika eneo la Eastlands viungani mwa mji mkuu, Nairobi.

Pia alishutumu polisi kwa kuwalenga wanahabari wakati wa maandamano dhidi ya serikali na kudai kulikuwa na mipango ya kushambulia afisi za Royal Media Services jijini Nairobi.

Bw Odinga alikosoa jumuiya ya kimataifa kwa madai ya kupuuza ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na mamlaka wakati wa maandamano hayo.

Alisema upinzani utafanya maandamano makubwa tarehe 3 Aprili kuishinikiza serikali kupunguza gharama ya maisha na kufanya mageuzi ya uchaguzi, miongoni mwa matakwa mengine.

Waandishi sita walijeruhiwa wakati wa maandamano ya Alhamisi, na kuongeza idadi ya watendaji wa vyombo vya habari waliojeruhiwa hadi 22 tangu maandamano hayo yalipoanza wiki iliyopita.

"Marekani inasikitishwa sana na ripoti za hivi karibuni za mashambulizi dhidi ya waandishi wa habari. Kulinda uhuru na usalama wa vyombo vya habari ni msingi wa demokrasia," balozi Meg Whitman alitweet Ijumaa asubuhi.

Pia unaweza kusoma:

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post