Polisi auawa Kenya baada ya kushambuliwa kwenye maandamano



Afisa wa polisi ambaye alijeruhiwa wakati wa maandamano ya kupinga serikali Alhamisi magharibi mwa Kenya amefariki.

Inspekta Jenerali wa Polisi Japheth Koome alisema Bernard Oduor alifariki alipokuwa akitibiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Alisema zaidi ya maafisa 20 wa polisi wamepata majeraha mabaya walipokuwa wakipambana na waandamanaji katika jiji la Kisumu lililo kando ya ziwa.

Katika taarifa, mkuu huyo wa polisi amelaani ghasia na uharibifu ulioshuhudiwa wakati wa maandamano ya upinzani katika mji mkuu, Nairobi na maeneo mengine ya nchi.

Wanahabari sita walijeruhiwa, na vifaa vyao kuharibiwa wakati wa maandamano ambayo yaligeuka kuwa ya vurugu kufuatia makabiliano kati ya waandamanaji na polisi.

Rais William Ruto amewakosoa waandamanaji hao akisema katiba haiwaruhusu kuhusika na ghasia.

Alisema maandamano ya kila wiki , kwa mara mbili yalikuwa na athari mbaya kwa uchumi na kuvuruga maisha ya watu.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga ameshutumu polisi kwa ukatili dhidi ya wafuasi wake na kuonya kuhusu kile alichokitaja kuwa "mama wa maandamano yote" Jumatatu ijayo.

Amedai kuwa maisha yake yako hatarini, akisema kuwa jaribio la mauaji lilifanywa dhidi yake.

Ingawa nyuma ya pazia juhudi za viongozi wa kdini na mjumbe wa Marekani wanaangalia namna ya kumaliza makubaliano huku pande zote mbili zikichukua misimamo mikali.

Soma zaidi:

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post