Klabu ya Simba imemtangaza Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Hemed Suleiman

 


Klabu ya Simba imemtangaza Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Hemed Suleiman maarufu kwa jina la Morocco kuwa Kocha wa muda wa Timu hiyo kwenye mechi za Kimataifa baada ya aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo Fadlu Davids kusitisha mkataba wake huku Kocha Selemani Matola akikosa sifa za kukaa benchi kutokana na kadi nyekundu.
Simba imethibitisha kuwa imepata kibali rasmi kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumruhusu Kocha Morocco kujiunga na Benchi la ufundi kwa muda wakati huu ambao Klabu ya Simba SC inakamilisha mchakato wa kumpata Kocha wa kudumu.
Morocco ataiongoza Simba katika mchezo muhimu wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United FC utakaopigwa Septemba 28, 2025.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post