‘Hatumuogopi rais’ Timu ya taifa ya Gambia yasusia kukutana na rais wa nchi Adama Barrow

 





Timu ya taifa ya soka nchini Gambia imesusia mkutano na Rais wa nchi hiyo Adama Barrow kufuatia mzozo kuhusu mafao yao ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.Wachezaji wameandika kwa Rais wa Shirikisho la Soka la Gambia (GFF) Lamin Kaba Bajo kukataa mwaliko wa kukutana na rais Jumatatu.

GFF haijajibu majaribio ya BBC Sport Africa ya kupata jibu kwa barua iliyotumwa na kikosi hicho.Katika mkutano huo wachezaji walitarajia Rais Barrow atakabidhi Dalasi milioni 11 (takriban $ 215,000) kugawanywa kati ya wachezaji wote na wafanyikazi wa kitengo cha kiufundi waliohusika katika kufuzu kwa Kombe hilo.

Kikosi hakihisi pesa zinazotolewa zinaonyesha ukubwa wa mafanikio yake na kina wasiwasi pia kwamba kukubali pesa hizo kutaweka mfano mbaya kwa siku zijazo."Timu ingependa kumshukuru Mheshimiwa kwa mwaliko huo lakini watakataa mwaliko wa kukutana na pesa zilizotolewa," barua hiyo ilisema."Kwa wachezaji, kuichezea Gambia haijawahi kuwa kuhusu pesa.

Badala yake, mara zote ilikuwa juu ya kupeperusha bendera ya Gambia na kuwapa watu wa Gambia fahari."Wachezaji walikuwa wakifurahia wito wa kuchezea timu ya taifa bila kutarajia au kuomba malipo yoyote, bila kujali ugumu ambao wakati mwingine unajitokeza"Soka ni mchezo wa motisha. Baada ya kufuzu kushiriki kombe la Mataifa ya Afrika mwakani kwa mara ya kwanza katika historia ya Gambia.

Timu inastahili kupewa bonasi ambayo itawatia motisha wachezaji na kila mtoto ambaye ana ndoto ya kuchezea Gambia. siku moja."Timu inahisi kwamba heshima na motisha waliyopewa wachezaji iko chini ya ile inavyotakiwa kuwa.

Kwa sababu hiyo, wachezaji kwa kauli moja waliamua kukataa mwaliko."Tunatumahi kuwa kwenda mbele, wachezaji watapewa motisha ya kutosha wakati maandalizi ya kombe la Afrika yanaendelea."

Gambia iliweza kufuzu kwa fainali za Kombe hilo mwezi Januari nchini Cameroon kwa kumaliza kileleni mwa kundi lao mbele ya Gabon, DR Congo na Angola.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post