Mahakama yatengua uamuzi wa Fatma Karume kufutiwa uwakili

 




Mahakama Kuu nchini Tanzania imetengua uamuzi wa kamati ya maadili ya mawakili wa kumfutia moja kwa moja uwakili mwanasheria Fatma Karume.

Pamoja na kutengua uamuzi huo, Mahakama hiyo imeagiza uamuzi huo uliotokana na malalamiko yaliyowasilishwa na mwanasheria mkuu wa serikali yarejeshwe kwenye Kamati hiyo ya Maadili na mwanasheria huyo apewe nafasi ya kujitetea.

Hata hivyo uamuzi huo haimaanishi amerejeshewa uwakili wake uliofutwa awali, isipokuwa anapaswa kwenda mbele ya kamati ya maadili ili kujitetea.

kwenye ukurasa wake wa Twitter Fatma ametaja uamuzi huo wa mahakama ingawaje amesema hajarejeshewa uwakili

Fatma Karume mtoto wa Rais mstaafu wa awamu ya sita Zanzibar, Aman Karume na mjukuu wa mtoto wa Rais wa kwanza wa nchi hiyo, Abed Karume alivuliwa uwakili mwaka 2019 kwa madai ya hatua yake ya kukosoauteuzi wa Mwanasheria Mkuu Dkt Adelarus Kilangi aliyeteuliwa na rais John Pombe Magufuli February, 2018.

Ingawa kujihusisha kwake kwenye siasa kunahusishwa na kadhia iliyomkuta.Baada ya uamuzi huo wa Mahakama, Fatma mbali na kutoa ufafanuzi wa kuhusu uamuzi huo kupitia mtandao wake wa Twitter amewashukuru pia watu mbalimbali akiwemo wanasheria waliomsimamia kesi yake hiyo akiwemo Peter Kibatala, Profesa Issa Shivji, Rugemaleza Nshala na Mike Ngale.

Kwa muda sasa Mwanasheria huyo amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali iliyo madarakani na amejitambulisha kama mwanamamke asiye muoga kusema chochote na popote.Kutokana na misimamo yake hiyo , ameshakutana na visa vya kuvamiwa na kuchomwa kwa ofisi yake ya uanasheria pamoja na kufukuzwa kwenye Taasisi moja ya kisheria aliyokuwa anafanya kazi.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post