Homebongo habari Je Illuminati ilianza wapi na kwanini? byben -June 20, 2021 0 "Nmesikia kuwa kuna vikao hapa, lakini ni wapi na muda gani, sijui ," Dada Anna aliniambia, chukua muda kufungua kwenye mada hii. "Nadhani wanatokea Ufaransa, Uingereza, na maeneo yote duniani lakini Ingolstadt ndio eneo la kukutania Ulaya."Kufanya kazi katika duka la vitabu la kanisani mkabala na kanisa kubwa la miujiza la Liebfrauenmünster, Dada Anna anaonana na kuzungumza na watu wengi.Lakini wengine wanabaki kuwa hawajui siri kubwa iliyopo: Mahujaji wa Iluminati, ambao anaamini kuwa bado huwa wanabeba siri nzito kutoka kwenye vikao katika mji wa Bavarian.Wazo kuwa washiriki wa Iluminati wanakusanyika kwa siri katika mji mdogo wa Bavarian unaonekana kuwa wa ajabu katika historia.Mji huu ni eneo ambalo kuna jamii ya siri kubwa ilizaliwa hapo ambayo imekuwa sehemu ya hadithi, sehemu ya ukweli wa historia na taasisi isiyokuwa na misingi katika nadharia zake.Ilikuwa Mei Mosi ,1776 Adam Weishaupt, profesa wa sheria katika chuo kikuu cha Ingolstadt, alibaini maelekezo ya Illuminati, siri ya taasisi ambayo ilikuwa imeanzishwa kupinga ushawishi wa kidini katika jamii na wanaotumia madaraka vibaya katika serikali kupata nafasi salama ya kukosoa, kujadiliana na kuwa na uhuru wa kujieleza.CHANZO CHA PICHA,(CREDIT: VOLKERPREUSSER/ALAMY)Maelezo ya picha,Mji ambao Iluminati ilianzishwaWalivutiwa na Freemasons na wanafilosofia wa Ufaransa, Weishaupt aliamini kuwa jamii haipaswi tena kuongozwa kwa mabavu na imani za kidini, badala yake alitaka kuunda eneo la uhuru na usawa ambapo maarifa hayakuzuiwa na matakwa ya kidini.Hata hivyo dini na sheria za kisiasa zilizoongozwa katika Ingolstadt wakati huo, jambo lililokuwa likifundishwa katika chuo ambacho Weishaupt alikuwa anafundisha lilkuwa na uangalizi wa hali ya juu.Baada ya kuchagua wanafunzi watano wenye vipaji katika sheria ili kujiunga, mtandao ukakuwa ghafla,wanachama wake wakatangaza malengo ya elimu hiyo, wakati huohuo wakiunda mtandao wa kutoa taarifa juu ya mwenendo wa nchi na viongozi wa dini katika jitihada utoaji taarifa ambapo Iluminati inaweza kufanikiwa katika mafundisho yake.Kwa msaada wa mwanadiplomasia maarufu wa Ujerumani Baron Adolf Franz Friedrich, Freiherr von Knigge - ambao walisaidia kuanzisha makazi ya Freemason kwa ajili ya Iluminati- makundi ya siri yalikuwa na kuwa zaidi ya wanachama 2,000 katika maeneo yote ya Bavaria, Ufaransa, Hungary, Italia na Poland, na kwingineko.CHANZO CHA PICHA,JULIE OVGAARDWakati katika mji ambao kila kitu kilianzia, yanafahamika machache na wenyeji."Si watu wengi wanafahamu kuhusu suala hilo . Lakini Iluminati ni sehemu ya historia ya Ingolstadt," mwandishi wa eneo hilo Michael Klarner alielezea wakati akiwa amesimama nje ya chuo kikuu cha Ingolstadt, akiwa hadhanii kuwa kanisa -ni sawa na kujenga katiba fupi kutoka kwa dada Anna wa duka la vitabu.Masuala ya Illuminati hayakuwekwa kwa malengo ya kutaka kujulikana"Weishaupt ilikuwa na mabadiliko mengi, Klarner aliendelea. "Alipenda wazo la kufundisha watu kuwa binadamu wema. Alitaka kubadili jamii, alikuwa anaota kuwa na dunia bora zaidi yenye serikali bora zaidi. Alianzisha wazo la Iluminati akiwa na wazo la ukarimu kwa binadamu inabidi ufundishwe - jambo ambalo lilikuwa haliruhusiwi katika chuo kikuu hicho."Kuingia katika jengo la chuo kikuu, nilikuwa naangalia ishara yeyote ya taasisi ya Weishaupt kuanzishwa katika eneo hilo, hakuna chochote kilichotambulisha suala hilo.CHANZO CHA PICHA,DR. WILFRIED BAHNMÜLLERLakini labda hilo lisishangaze sana-Iluminati haikutaka kujulikana kabisa.Hata hivyo taasisi hiyo haikuwezekana kuwa ya siri kwa muda mrefu.Muongo mmoja tu baada ya kuanzishwa kwake, jamii hiyo ya siri iliingiliwa na mamlaka ya Bavarian baada ya kuandika maelezo ambayo yalikamatwa na mamlaka ya serikali.Illuminati ilifungwa na Weishaupt aliondolewa Ingolstadt na kuishi maisha yake yote Ujerumani katika mji wa Gotha, kilomita 300 kuelekea kaskazini.Ingawa wazo hilo la jamii ya siri lilikuwa baya dhidi ya nchi liliweka mawazo mabaya tangu kuanzishwa kwake, muhtasari wa nadharia za njama zilizopikwa na wale ambao wanaamini kuwa Illuminati haikusambaratishwa kabisa - ulidai kuwa wanahistoria walikuwa wamewaanika kwa kiasi kikubwa.Hata mipango yao katika taasisi ambayo walikuwa wanaifanyia kazi kwa siri ilihojiwa na mamlaka. Iluminati ilikuwa imechukuliwa kuwa sehemu ya mapinduzi ya Ufaransa, wakishirikiana na rais wa Marekani John F Kennedy na hata shambulio la kigaidi la Septemba 11, 2001, na amekuwa maarufu kupitia vitabu na filamu kama Dan Brown Angels na mashetani. Tags bongo habari Facebook Twitter