Homebongo habari Myamar yapinga azimio la UN kuhusu vikwazo vya silaha. byben -June 20, 2021 0 Myamar yapinga azimio la UN kuhusu vikwazo vya silaha.Wizara ya mambo ya nje ya Myanmar imepinga azimio la baraza kuu la Umoja wa Mataifa la kutaka taifa hilo kuwekewa vikwazo vya silaha na pia kulishtumu jeshi la nchi hiyo kwa kuchukuwa mamlaka mnamo mwezi Februari. Myanmar imelitaja azimio hilo lililopitishwa siku ya Ijumaa kuwa lisilokuwa na mashiko kisheria kwa sababu limezingatia madai ya upande mmoja na nadharia za uongo. Katika taarifa iliyotolewa na wizara hiyo mjini Naypyitaw, wizara hiyo imetuma barua za pingamizi kwa katibu mkuu wa umoja wa Mataifa na pia rais wa baraza kuu la Umoja huo. Azimio hilo liliakisi mtazamo mmoja wa jumuiya ya kimataifa dhidi ya mapinduzi ya kijeshi yalioiondoa madarakani serikali ya Aung San Suu Kyi iliyochaguliwa kidemokrasia. Azimio hilo lilitoa wito kwa uongozi wa kijeshi kurudisha mchakato wa mpito wa kidemokrasia nchini Myanmar, na pia lililaani matumizi ya nguvu za ziada kukandamiza maandamano yaliyofuatia mapinduzi, huku likitoa wito kwa mataifa yote kuzuia uingizaji wa silaha nchini humo. Tags bongo habari Facebook Twitter