Homebongo habari Serikali yatenga Sh2 bilioni ujenzi shule ya kata Misungwi byben -June 14, 2021 1 Mwanza. Serikali ya Tanzania imetenga Sh2.4 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa shule ya kata ya Misungwi.Akiwasalimu wakazi wa Misungwi wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na usafi wa mazingira wa mji wa Misungwi, Waziri wa Tamisemi, Ummy Mwalimu amesema fedha hizo zitatolewa Julai, 2021.Akizungumza leo Jumatatu Juni 14, 2021 amesema kwa kuanzia shule hiyo itakuwa na madarasa manne, maabara tatu na nyumba mbili za walimu.Amesema walimu 677 wa wilaya hiyo tayari wameshaingizwa kwenye mfumo wa kupanda madaraja na kwamba ambao hawajaingia kwenye mfumo huo ni walimu 36 tu.Katika kuboresha huduma za afya, Ummy amesema tayari Sh544 milioni zimeshatengwa kwa ajili ya kuboresha huduma hizo wilayani Misungwi na Sh800 milioni imeshatengwa kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Misungwi. Tags bongo habari Facebook Twitter