Homebongo habari Tahadhari ya corona wananchi wakimsubiri Samia byben -June 14, 2021 0 Mwanza. Wananchi waliojitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa mradi wa maji wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza wamehimizwa kuvaa barakoa na kunawa mikono kwa maji tiririka kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19.Uzinduzi wa mradi huo wenye mitambo ya kusukuma lita milioni 4.5 za maji safi na salama utafanywa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu Juni 14, 2021.Mwananchi Digital limeshuhudia wananchi wakihimizwa kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kunawa mikono kwa tiririka na sabuni katika maeneo yaliyotengwa kwenye kila geti la kuingilia eneo hilo.Huku wakiendelea kumsubiri Rais Samia kwa ajili ya uzinduzi wa mradi huo uliogharimu zaidi ya Sh39.7 bilioni, wananchi wameonekana wakiwa wamevaa barakoa wakati wote.Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zaidi ya watu 175,306,598 wamekutwa na maambukizi ya virusi hivyo duniani huku 3,792,777 wakifariki kwa ugonjwa huo hadi kufikia Juni 13, 2021. Tags bongo habari Facebook Twitter