Wahubiri wanaookoa 'miungu' iliyokataliwa Nigeria

Reverend Paul Obayi holds an idol

CHANZO CHA PICHA,OKUNERERE

Muhubiri mmoja wa kanisa katoliki anaendesha jumba la makumbusho mashariki mwa Nigeria ili kuhifadhi masanamu na vifaa vingine vinavyochomwa na wahubiri wenzake wa kanisa la Pentecostal ambao wanaziona kama njia ya kuabudu sanamu.

Masanamu hayo ni miongoni mwa tamaduni za kidini ambazo watu wa kabila la Igbo huyafanya kuwa sehemu ya ibada zao.

Huyaona masanamu hayo kuwa matakatifu na kuwa na nguvu zisizokuwa za kawaida.

Lakini kuna wafuasi wachache kwa sasa wa tamaduni hizo, huku dini za Kikristo na hususan kanisa la Pentecostal likiendelea kukuwa.

Wanahabari wa Idhaa ya BBC Igbo, Chiagozoe Nwonwu na Karina Igonikon waliandika kuhusu jaribio la wahubiri wa kikatoliki kuyalinda masanamu hayo, kutoka kwa wahubiri wa kanisa la Pentecostal.

Huku yakipatiwa jina la 'moto unaochoma' , hakuna kitu kinachoogofya kuhusu mhubiri Paul Obayi , ambaye anaendesha jumba la makumbusho la Deities katika mji wa mashariki mwa Nigeria wa Enugu.

Likiwa ndani ya kanisa la katoliki la mtakatifu Mary, jumba hilo la makumbusho lenye vyumba vitatu, lina mamia ya vinyago na simba waliochongwa - vyote hivyo vikiwa ni miongoni mwa utamaduni za watu wa igbo.

Baada ya jamii kuwacha imani za jadi kutokana na ushawishi wa makanisa ya Pentecostal, baadhi ya wahubiri huchoma moto masanamu hayo ambayo yanaonekana kwenda kinyume na imani ya dini hiyo na kuvutia mapepo yanayoleta bahati mbaya.

Mara nyengine waumini wa dini hizo za kitamaduni pia huyachoma masanamu yao kulingana na imani iliyopo katika kabila la Igbo kwamba: Iwapo mungu anasumbua sana, anakuwa mbao ya kuchomwa.

Michongo ya mbao inayoliwa na wadudu

Mhubiri Obayi anaunga mkono uhifadhi wa sanamu hizo, akisema anatumia uwezo wake wa kidini kuondoa uwezo wao. hatua iliomfanya kupewa jina la Okunerere - "Moto unaochoma sanamu".

"Nimeharibu mapepo'' , alisema katika mahojiano katika jumba hilo la makumbusho.

Kile ulichonacho sasa ni ganda tupu hakuna kitu ndani yake."

Sanamu nyingi katika makavazi hayo zimetokana na mbao
Maelezo ya picha,

Masanamu mengi katika makavazi hayoyametokana na mbao

1px transparent line

Mhubiri Obayi alisema kwamba ameshawishiwa na makavazi katika mataifa ya magharibi, ambayo yamekuwa katika shinikizo kali kurudisha vitu vya kale kama vile shaba ya Benin ambazo ziliibiwa wakati wa ukoloni.

"Hutembelea makavazi katika mataifa ya magharibi na naona vitu vya kale kutoka Benin, na nikaamua kuhifadhi vyetu," alisema Obayi .

Mungu wa uzazi

Na msimamizi wa kanisa la Cathedral, mhubiri Eugene Odo, anaunga mkono mpango huo.

''Katika siku za usoni watu watatazama nyuma na kuona jinsi tulivyotengeneza vipande vya mbao na kuviita mungu wetu," alisema..

Vitu hivyo vya kale baadhi yao vikiwa na umri mkubwa na vimetapakaa katika sakafu ya makavazi hayo, vikiwa na vumbi, vingine vimeharibiwa na wadudu.

Vifaa hivyo vinatoka katika huduma ya ukombozi ambayo amekuwa akiitekeleza kwa kipindi cha miaka 20 iliopita katika miji na vijiji kusini mashariki mwa Nigeria.

"Watu huandika barua wakilqitaka kanisa langu kuja kuondoa sanamu ambazo zinawasumbua," alisema.

Mashariki mwa Nigeria, Odinani, dini ya zamani ya kanila la igbo ilikuwa ikifuatwa kabla ya kuwasili kwa Ukristo na wakoloni.

Ni mfumo wa uhuishaji ambapo watu huomba kwa pepo - zinazowakilishwa na sanamu kwa jina Chi.

Sanamu hilo huomba kwa niaba ya binadamu au Chukwu. Sanamu nyengine zinazoabudiwa ni pamoja na :

  • Ala - mungu wa uzazi
  • Amadioha - mungu wa radi
  • Ekwensu - Mungu wa biashra na ubaya

Ni waumini wachache wa dini hizi za kale waliosalia na hushutumiwa pakubwa na wakristo walio wengi.

Getty Images

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

1px transparent line

Chinasa Nwosu, askofu wa Pentekostal wa kanisa la Royal Church katika mji wa kusini wa Port Harcoiurt amekuwa mkosoaji mkubwa wa imani hizo.

Askofu Nwosu kwa mara ya kwanza alijipatia umaarufu mapema miaka ya tisini kwa kuharibu maeneo matakatifu , kuchoma sanamu hizo na kung'oa miti alioitaja kuwa ya mapepo wachafu.

Baadhi yao ilikuwa imekaa kwa miaka mingi na kutumika kama ishara za uhuishaji.

"Mungu hataki sisi kuabudu sanamu . Dini nyingi za Afrika zinapendelea kuabudu masanamu," alisema..

"Baraka huja unapoondoa sanamu zilizolaaniwa,'' aliongeza akinukuu bibilia.

Bishop Chinasa Nwosu anachoma sanamu ambazo anaamini ni kinyume na mafunzo ya kikristo

CHANZO CHA PICHA,THE ROYAL CHURCH

Maelezo ya picha,

Askofu Chinasa Nwosu anachoma masanamu ambayo anaamini ni kinyume na mafunzo ya Kikristo

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post