Fahamu mambo 7 kuhusu ubongo wako ambayo yamekuwa yakitajwa lakini sio ya kweli

ubongo

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Kuna mawazo ambayo hukaa kwa muda mrefu kwasababu yana uwezo kubaini dhana za ajabu huku mengine yakiwa hayawezi kuepuka ukali wa kisayansi.

Katika karne ya 4 Aristotle alichukulia ubongo kama kiungo cha pili ambacho kilitumika kupoza damu ambayo moyo ulitumia kwa kazi zake za kiakili.

Baada ya utafiti wa muda mrefu, daktari wa maungo kutoka Roma Galen (c. 130-c. 210 BK) alihitimisha kuwa akili ilizalishwa kikamilifu katika ubongo na sio moyoni, kama Aristotle alivyopendekeza.

Katika karne ya 16, wakati Leonardo da Vinci alipokuwa akichora na kuusoma ubongo, moja ya malengo yake ilikuwa kupata eneo ulipo; wanafalsafa kama Thomas Aquinas, Locke, na Kant walichunguza; saikolojia, waliikubali, na wanasayansi waliendelea kujaribu dhana ya hisia hiyo ya sita ambayo husafisha habari ya kile wanachokiona na hisia tano hadi leo.

Ubongo ambao umetajwa kuwa uumbaji wa kipekee kama mwanasayansi wa Denmark Nicolaus Steno alivyosema 1969 ni mojawapo ya uwanja wa maarifa ya uwongo na yalio sahihi.

Kwa kuwa hatuko huru kuwa na baadhi yao, tuliwasiliana na mwanasayansi mashuhuri wa fizikia Lisa Feldman Barrett, mwandishi wa "Masomo Saba na Nusu kuhusu Ubongo," ambayo yeye huonyesha "nafasi kubwa ya kijivu iliopo kati ya masikio yetu."

Tulimuuliza kwa mfano iwapo ni kweli kwamba sisi huzaliwa na idadi kadhaa ya niuroni ambazo ndio tunazokuwa nazo kwasababu hazizaani kama seli nyengine za mwili wa mwanadamu.

½. Neuroni ndogo

Hii inakaribia kuwa kweli.

"Binadamu wamepoteza uwezo kuzalisha Niuroni , isipokuwa katika maeneo kadhaa ndani ya ubongo'', anasema mwanasayansi wa niuroni,"

Na sio hilo tu…

Niuroni

Ubongo wa mwanadamu unavyofanya kazi

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Ubongo wa mwanadamu unavyofanya kazi

"Wanyama wanaoishi kwa muda mrefu hupoteza kiwango hiki kwasababu wakati niuroni zinapobadilisha niuroni zilizozeeka, watu hupoteza fahamu. Cha kushangaza ni kwamba kuna Wanyama wanaozalisha niuroni katika kipindi chote cha uhai wao.

Ndege wanashangaza sana kwasababu kuna baadhi ya maeneo katika ubongo wao ambapo Niuroni zinazaana kila mwaka ili kujifunza nyimbo mpya za kuvutia wapenzi.

1.Niuroni zilizopotea

Niuroni

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Madai ya kwamba tunatumia asilimia 5 au 10 pekee ya niuroni zetu sio kweli.

Fikiria kupoteza asilimia 90 ya uwezo wako ! ni vigumu sivyo ilivyo.

"Tunatumia ubongo kila wakati na sio niuroni moja lakini mamilioni na mamilioni kwa kila wakati."

Hakika, kuhifadhi kila kitu ambacho akili zetu zinaona kuwa sawa.

2. Macho yako yanaona masikio yako yanasikia na ngozi yako inahisi

Sio kweli.

Hisia zetu zote ni tafsiri ya ubongo.

ubongo unavyofanya kazi kama mashine

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Ubongo unavyofanya kazi kama mashine

"Unahitaji aina fulani ya uso wenye hisia, aina fulani ya kipokezi, ili kubeba habari kwenda kwenye ubongo", kama masikio, ngozi, pua, na macho.

Lakini ishara hizo - mawimbi ya mwangaza, sauti - ambazo hupokea hazina maana hadi ubongo utakapotengeneza.

"Ndio maana kuna hali kama upofu wa gamba, ambapo macho hufanya kazi vizuri, lakini kuna uharibifu katika sehemu ya ubongo ambayo ni muhimu kwa kumfanya mtu aweze kuona."

Hauoni kwa macho yako, wala husikii kwa masikio yako, wala haujihisi kwa ngozi yako: unafanya hivyo kwa kutumia ubongo wako, ambao unachanganya kile kilicho kichwani mwako na data ya hisia inayogunduliwa na viungo vyako.

Na sio hiyo pekee...

3. Hisia zako ziko moyoni mwako

Wakati hisia zinakuvamia, "unapohisi mapigo ya moyo wako, hauyasikii kwenye kifua chako, lakini kichwani mwako."

"Ni vigumu kuelewa lakini hauhisi chochote mwilini mwako, kile unachohisi kiko kwenye ubongo wako."

Maumivu, furaha ... kila kitu, kwa sababu ubongo, ndio msimulizi.

4. Una mnyama wa ndani

Hata ... sio kweli.

Ubongo unoafanya hesabu

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Ubongo unoafanya hesabu

Ni kweli kwamba kuna mfano unaojulikana kama "ubongo wa utatu", ambao una muundo wa reptilia, mfumo wa limbic na neocortex, na jukumu lake la kwanza ni kudhibiti na fikira za asili kuishi, wa pili anayehusika na kudhibiti mhemko, kumbukumbu na uhusiano wa kijamii, na wa tatu, anayehusika na kazi za kisasa zaidi.

Wazo ni kwamba ubongo wako ni uwanja wa vita kati ya mnyama wako wa ndani na nafsi yako ya busara ya hali ya juu.

Maelezo ya video,

Zanzibar:“Baba aliniambia nilale chini kisha akaniingilia, na mama akasema ninyamaze'

Wakati busara inashinda, wewe ni mwadilifu na mzuri na mwenye afya lakini mnyama wako wa ndani akishinda, wewe ni mbaya, kwa sababu hukujaribu sana au unaumwa, kwa sababu busara haikuweza kudhibiti mnyama wako wa ndani.

''Simulizi zote hizo ni hadithi.

"Lakini kinachofurahisha sana ni kwamba maeneo ya ubongo ambayo yametajwa kama mnyama wako wa ndani ndio yanayodhibiti mwili wako - mapafu yako, moyo wako, kinga yako, metaboliki yako ... kwa jumla mwili wako wote.

"Viungo hivyo vinahusika kwa kila kitu katika ubongo wako." Hivyobasi hutumika katika jukumu muhimu la ubongo ambalo ni kufikiria?

5. Ubongo ni wa kufikiria

Ubongo unaofikiria

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Unapofikiria kuhusu umuhimu wa ubongo unaweza kujibu, kufikiria, ama kuhisi ama uwezo wa kuuchukulia ulimwengu. "

"Ukweli ni kwamba kazi muhimu ya ubongo ni kuishi . Kufikiria, kuhisi na kuchukulia ili kuweza kudhibiti mfumo wa ndani wa mwili wako ili uendelee kuishi , kusalia na afya njema, na kuendelea kuzaa ".

6. Ubongo wako hujibu

Moja ya vitu ambavyo vilimshangaza Lisa Feldman Barrett zaidi ni kujifunza kuwa ubongo hufanya kazi kupitia utabiri.

"Sikuamini kwa sababu situmii muda wangu kufanya utabiri na kisha kujibu lakini nikipata kitu na kujibu wakati huo.

"Lakini ukweli ni kwamba haujali mambo ya ulimwengu.

"Ubongo wako unaendesha muundo wa ndani ambao umejifunza dharura za ishara za hisia ambazo zimefunuliwa kwa maisha yake yote, na kila wakati unabashiri ni nini kitatokea.

"Unafanya hivyo moja kwa moja, ukirusha ishara kutoka kwa niuroni zake kutarajia data ya hisia kutoka kwa huduma zake za hisia. Halafu wakati data inapoingia, inalinganisha''.

Mionzi ya ubongo

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mionzi ya ubongo

"Sio kwamba hujawahi kupata vitu vipya lakini hauyashangazi maisha yako yote''.

"Wakati kuna mshangao, kilichotokea ni kwamba ubongo wako umejaribu kutabiri, kama kawaida, lakini ishara hizo hazitabiriki, na hiyo inakuwa fursa ya kujifunza kitu kipya."

Na hatimaye….

7. Ubongo wako unafanya kazi peke yake

Inatokea kwamba ubongo wako hufanya kazi kwa siri na bongo za watu wengine .

Familia yako, marafiki, majirani, na hata wageni huchangia muundo na utendaji wa ubongo wako na kusaidia kufanya mwili wako ufanye kazi.

Majaribio yameonyesha kuwa mabadiliko katika mwili wa mtu mmoja mara nyingi husababisha mabadiliko kwa mwingine, iwe ni wawili wanaohusika kimapenzi, marafiki tu, au wageni wanaokutana kwa mara ya kwanza.

Unapokuwa na mtu unayemjali, kupumua kwako kunalinganishwa, pamoja na mapigo ya moyo wako. Aina hii ya uhusiano wa mwili hufanyika kati ya watoto wachanga na walezi wao, kati ya wataalamu na wateja wao, na kati ya watu ambao huchukua darasa la yoga au wanaimba pamoja kwenye kwaya.

Maelezo ya video,

Jeshi la Marekani lathibitisha uwepo wa viumbe wa ajabu angani

Ikiwa, badala yake, watu hawahurumiani, akili zao ni kama wenza katika densi ambapo hawaachi kukanyagana miguu.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post