Freeman Mbowe:Polisi wasema Kiongozi wa upinzani alipanga kutekeleza vitendo vya kigaidi ikiwemo kuua viongozi wa serikali


Freeman Mbowe

CHANZO CHA PICHA,AFP

Maelezo ya picha,

Mbowe pamoja na wenzake 11 kutoka chama cha Chadema walikamatwa na polisi usiku wa kuamkia Jumatano jijini Mwanza.

Polisi nchini imesema Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe anakabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwemo za kupanga njama za kufanya vitendo vya kigaidi na kuua viongozi wa Serikali.

Taarifa ya Msemaji wa Polisi, David Misime imesema kuwa Mbowe hakukamatwa kwa tuhuma za kupanga na kuandaa kongamano la Katiba mpya jijini Mwanza bali alifahamu tuhuma zinazomkabili .

"Mbowe alikuwa anafahamu fika kuwa tuhuma zinazomkabili zilikuwa zinachunguzwa na wakati wowote angehitajika Polisi kwa hatua za kisheria mara tu uchunguzi wake utakapokamilika. Hatua hiyo imefikiwa sasa," alisema Misime.

Taarifa iliyotmwa na polisi inasema washukiwa sita tayari wamefikishwa kortini kwa tuhuma hizo .Taarifa hiyo imeongeza kuwa uchunguzi unaoendelea Mwanza na Iwapo itabainika kwamba Mbowe na wenzake wanaoshikiliwa walivunja sheria basi watachukuliwa hatua zifaazo .

Kiongozi huyo wa upinzani amekuwa chini ya ulinzi wa polisi kwa siku mbili na mapema leo polisi ilithibitisha kumkamata .

Mkuu wa polisi wa Mwanza, Ramadhan Ng'anzi alisema walikuwa wakimzuilia Mbowe kwa mahojiano Zaidi .

RPC Ng'anzi alisema kiongozi huyo wa upinzani alikamatwa siku ya jumatano katika hoteli ya Kingdom Hotel kwenye barabara ya Ghana

"Tulipomkamata ,polisi wa kanda maalum ya Dar es salaam walituarifu kwamba walikuwa wakimtafuta kwa uhalifu mwingine aliotekeleza huko ,kwa hivyo tulimsafirisha hadi Dar es Salaam ambako anaendelea kuhojiwa' Kamanda huyo alisema

Mashirika ya kutetea haki yakosoa kukamatwakwa Mbowe

Mashirika yanayotetea haki za binadamu yameikosoa vikali hatua ya Jeshi la Polisini nchini Tanzania ya kuwakamata baadha ya viongozi wa chama cha upinzani nchini humo Chadema.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania na shirika kimataifa la Amnesty International ni miongoni mwa waliojitokeza na kupinga hatua hiyo.

Kwa upande wake, Amnesty International imeitaka serikali kusitisha mara moja kile ilichokiita kuendelea kudhibitiwa kwa upinzani nchini Tanzania.

Wito huu uliotolewa na mashirika haya, unakuja baada ya viongozi na wanachama kumi na mbili akiwemo kiongozi mkuu wa Chadema Freeman Mbowe kutiwa mbaroni huko jijini Mwanza usiku wa kuamkia tarehe 21 mwezi Julai.

Kauli za hivi karibuni za Bw Mbowe

Mwanzoni mwa wiki hii kiongozi wa Chadema Freeman Mbowe alifanya mkutano na waandishi wa habari ambapo alilalamikia kukamatwa kwa wafuasi wa chama hicho na polisi, pamoja na suala la mabadiliko ya katiba.

Chama kikuu cha Upinzani nchini Tanzania, CHADEMA kimesema hakitaendelea kumpigia magoti Rais wa nchi hiyo, Samia Hassan Suluhu kuhusu mustakabali wa taifa hilo, Bw Mbowe aliwaambia waandishi wa habari hivi Jumatatu.

Mwenyekititi huyo wa CHADEMA, aliyasema hayo kufuatia Jeshi la Polisi la nchi hiyo kuwakamata viongozi, wanachama wa chama hicho pamoja na viongozi wa dini 38 waliokuwa wahudhurie mkutano wa chama hicho kupitia baraza lake la vijana (BAVICHA) wenye lengo la kuhamasisha kupatikana kwa katiba mpya ya nchi hiyo.

Mara baada ya kuingia madarakani mwezi Machi mwaka huu, Rais Samia alitangazia umma dhamira yake ya kukutana na wapinzani ili kuzungumzia maswala mbalimbali ikiwemo ya kisiasa na namna gani ya kuendesha shughuli za siasa.

Licha ya kukutana na makundi mengine kama vijana, wazee na wanawake mpaka sasa Rais Samia hajakutaa na wapinzani. ''Hatuwezi kuendelea na ule utaratibu wa zamani, tuna haki ya kukutana tunakamatwa, tunapigwa, tunashitakiwa, tunasoteshwa mahakamani miaka miwili miaka mitatu, kisha tunaachiwa huru, ama tunahukumiwa vifungo batili tukikata rufaa sote tunashinda', alisema Mbowe

Pamoja na polisi kuzuia mkutano huo uliokua ufanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Boma wiki hii na kukamata watu hao 38, Kiongozi huyo wa Upinzani alisema, mkutano upo pale pale na utafanyika wiki hii na kama kukamatwa wako tayari kukamatwa wote.

Kama wanataka kuwaweka ndani wanachadema kwenye hoja hii ya katiba, wapanue kwanza na magereza, kwa sababu tuko tayari wote tuwekwe ndani , na wala hatutaomba dhamana' alisema Mbowe kabla ya kulaani kitendo cha Jeshi la Polisi Mwanza, kuwakamata viongozi wa dini na wafuasi wa chama hicho .

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post