Hafla ya ufunguzi ya Olimpiki kuhudhuriwa na watu chini ya 1,000




Hafla ya ufunguzi rasmi wa michezo ya Olimpiki mjini Tokyo inafanyika hii leo huku michezo hiyo ikiwa imegubikwa na wingu la maambukizi ya virusi vya corona. Hafla hiyo ya ufunguzi ambayo kawaida hushuhudia maelfu ya watu mashuhuri kuhudhuria, safari hii itakuwa na chini ya watu elfu moja. Michezo hiyo ilikuwa imeahirishwa kwa mwaka mmoja na mwaka huu waandalizi walichukua hatua ya michezo hiyo kufanyika bila mashabiki uwanjani. Waziri Mkuu wa zamani wa Japan Shinzo Abe aliyechangia pakubwa kwa Japan kupata nafasi ya kuandaa michezo hiyo hatokuwepo katika ufunguzi wake pamoja na wadhamini kadhaa wakuu na viongozi wa kiuchumi ambao wanapinga kufanyika kwa michezo hiyo ya Olimpiki kutokana na janga la virusi vya corona.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post