Madai ya Taliban kudhibiti asilimia 90 ya mipaka ni uongo mtupu
Wizara ya ulinzi ya Afghanistan inasema madai ya kundi la Taliban kwamba linadhibiti asilimia 90 ya maeneo ya mpakani ya nchi hiyo ni uongo mtupu. Naibu msemaji katika wizara hiyo Fawad Aman ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP siku moja baada ya Taliban kutoa madai hayo kwamba, kauli hiyo ni propaganda isiyokuwa na msingi. Madai hayo ya Taliban yanatolewa baada ya kundi hilo kuyateka maeneo kadhaa ya mpaka wa Afghanistan na Iran, Tajikistan, Turkmenistan na Pakistan katika wiki za hivi karibuni. Haya yanafanyika wakati kundi hilo likiwa linaendelea kufanya mashambulizi makali kufuatia majeshi ya Marekani kuanza kuondoka nchini humo.
Tags
bongo habari