Mizozo Nigeria: Fahamu vitisho vitano vya usalama vinavyoikabili Nigeria

 

nigeria

CHANZO CHA PICHA,AFP

Nigeria inakabiliwa na wimbi lisilokuwa la kawaida la mizozo ya kiusalama - kuanzia utekaji nyara hadi wanamgambo wenye msimamo mkali - karibu kila pande ya nchi hiyo imekumbwa na vurugu na uhalifu.

Audu Bulama Bukarti, mchambuzi mwandamizi kuhusu suala la usalama wa Sahel katika Taasisi ya Tony Blair, amesema kiwango cha ukosefu wa usalama kinatishia msingi wa jamii ya Nigeria: "Kwa kila shambulio, maisha ya binadamu yanapotea au kuharibiwa kabisa na imani katika demokrasia nchini humo inapungua".

Wakati Rais Muhammadu Buhari alipochaguliwa mnamo 2015, aliahidi kulinda raia kutokana na magaidi na wahalifu. Lakini ikiwa imesalia chini ya miaka miwili muhula wake madarakani kumalizika,nchi imeendeea kutokuwa na utulivu ikilinganishwa na ilivyokuwa kwa miongo kadhaa. Wengine wamehusisha kuongezeka kwa ukosefu wa usalama hivi karibuni na kiwango cha umaskini mkubwa kote nchini humo. Ukosefu wa ajira kwa vijana kwa sasa hivi ni asilimia 32.5 na nchi iko katika moja ya nyakati mbaya zaidi ya kuporomoka kwa uchumi katika kipindi cha miaka 27 iliyopita.

Fahamu vitisho vitano vikubwa zaidi vya kiusalama Nigeria:

map

Licha ya kudai wakati wa mwaka wake wa kwanza madarakani kwamba kikundi cha wanamgambo wa Kiislamu cha Boko Haram "kilishindwa", Rais Buhari sasa anakubali kwamba serikali yake inashindwa kuzuia uasi, ambao ulianza kaskazini mashariki.

Ukweli ni kwamba, kundi la Boko Haram linaenea katika maeneo mapya na linatumia umaskini uliopo nchini Nigeria na changamoto zingine za usalama kuchochea itikadi zake za msimamo mkali.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa (UN), hadi mwisho wa 2020, mzozo na kundi hilo ulisababisha vifo vya karibu watu 350,000 na kulazimisha mamilioni ya wengine kukimbia makazi yao. Kikundi cha Boko Haram kilianzisha uvamizi mbaya katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo, wakati mwingine ikipandisha bendera yake na kuweka sheria kali kwa watu wa eneo hilo.

wakulima

CHANZO CHA PICHA,AFP

Maelezo ya picha,

Wakulima kadhaa walishambuliwa

Pia linatoza ushuru kwenye mashamba na uuzaji wa bidhaa za kilimo.

Soko la samaki la kimataifa lililokuwa wakati fulani linavuma katika neo la Bonde la Chad sasa linadhibitiwa kabisa na kikundi hilo.

Mapigano kati ya wafugaji na wakulima

Kumekuwa na mzozo mkali kati ya wafugaji wa kuhamahama na wakulima nchini Nigeria kwa miaka mingi.

Lakini kutokukubaliana juu ya utumiaji wa ardhi na maji, pamoja na sehemu za malisho, kumezidishwa na mabadiliko ya hali ya hewa na kuenea kwa Jangwa la Sahara, wakati wafugaji wanaposonga zaidi kusini kutafuta malisho.

Maelfu wameuawa katika mapigano ya kugombea rasilimali ambazo ni chache.

map

Jimbo la Benue, katikati mwa nchi, limerekodi mashambulio mabaya zaidi. Hivi karibuni, watu saba waliuawa wakati watu wenye silaha walipofyatua risasi kwenye kambi kwa wale waliokimbia mzozo.

Wengine pia wamelaumu wafugaji kwa utekaji nyara wa watu na kudai fidia.

m

CHANZO CHA PICHA,AFP

Wasiwasi huo umesababisha baadhi ya magavana wa serikali kupiga marufuku malisho kwenye ardhi za wazi, na hivyo kusababisha msuguano na serikali kuu. Mwaka 2019, mamlaka ya shirikisho ilizindua Mpango wa Kitaifa wa Mabadiliko ya Mifugo wa miaka 10 kupunguza kuhamisha ng'ombe kutoka sehemu moja hadi nyingine na kuongeza uzalishaji wa mifugo kwa jaribio la kumaliza mzozo.

Lakini wakosoaji wanasema ukosefu wa uongozi wa kisiasa, utaalam na ufadhili, pamoja na ucheleweshaji kunaharibu mpango huko.

Ujambazi na utekaji nyara

Moja ya vitisho vibaya vya kutisha familia nchini Nigeria ni utekaji nyara wa watoto wa shule mara kwa mara kutoka madarasani na nyumba zao za bweni. Zaidi ya wanafunzi 1,000 wametekwa nyara kutoka kwa shule zao tangu Desemba 2020, wengi wao wakiachiwa huru baada ya maelfu ya dola kulipwa kama fidia. Baadhi ya watekaji nyara hujulikana kama "majambazi" nchini Nigeria. Wahalifu hawa huvamia vijiji, huwateka nyara raia na kuchoma nyumba.

watoto

Mashambulio yanayotekelezwa na wavamizi hao yamelazimisha maelfu ya watu kutoroka makazi yao na kutafuta makazi katika maeneo mengine ya nchi. Kaskazini-magharibi kumekuwa kitovu cha mashambulio haya. Katika jimbo la Zamfara pekee, zaidi ya watu 3,000 wameuawa tangu 2012 na mashambulizi bado yanaendelea. Mamia ya shule zilifungwa kufuatia utekaji nyara katika shule za Zamfara na jimbo la Niger, ambapo watoto wenye umri wa miaka mitatu walikamatwa. Kwa kila dalili inayojitokeza, tasnia yenye faida kubwa ya utekaji nyara ya Nigeria inaendelea kustawi - na kusambaa hadi maeneo yaliyokuwa salama hapo awali - na hata kuonekana kushindwa kudhibitiwa. Hali hiyo imekuwa tishio kweli kwa biashara na elimu, na pia jamii za wakulima nchini.

Waasi wanaotaka kujitenga

Kikundi kinachotaka kujitenga kiitwacho Watu wa Asili wa Biafra kimekuwa kikipambana na vyombo vya usalama vya Nigeria.Kundi hilo linataka eneo fulani kusini-mashariki lenye watu kutoka kabila la Igbo, wajitenge na kuunda taifa lao huru la Biafra. Kundi hilo lilianzishwa mnamo mwaka 2014 na Nnamdi Kanu, ambaye alikamatwa hivi karibuni ambaye ana kabiliwa na mashtaka ya ugaidi na uhaini.

Kukamatwa kwake kumekuwa pigo kubwa kwa kundi hilo.

Wazo la Biafra kutaka kujitenga sio jipya

m

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mnamo mwaka 1967, viongozi wa eneo hili walitangaza serikali huru, ambayo ilisababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe vya kikatili na vifo vya idadi ya watu hadi watu milioni. Wafuasi wa Nnamdi Kanu wameshutumiwa kwa kuanzisha mashambulio mabaya dhidi ya ofisi za serikali, magereza, nyumba za wanasiasa na viongozi wa jamii.

Hata hivyo, Rais Buhari ameapa kuangamiza kundi hilo. Mwezi uliopita aliandika kwenye mtandao wa Twitter, "Wale wenye tabia mbaya" watashughulikiwa kwa lugha watakayoelewa. Ujumbe huo ulifutwa na mtandao wa Twitter kwa kukiuka sheria baada ya Bw. Buhari kukabiliwa vilivyo mtandaoni.

Tukio hilo lilipelekea kusitishwa kwa mtandao wa Twitter nchini Nigeria.

Waasi wa mafuta

nigeria

CHANZO CHA PICHA,AFP

Katika eneo la uzalishaji wa mafuta la kusini, changamoto za usalama sio kitu kipya. Ni eneo kubwa la uuzaji wa mafuta nje ya Nigeria, na wanamgambo katika eneo la Niger Delta kwa muda mrefu wamekuwa wakipigania kupata sehemu kubwa ya faida.

Wanasema kiwango kikubwa cha mafuta hutoka katika eneo lao na uharibifu wa mazingira uliosababishwa na uchimbaji wake umeharibu jamii na kuwafanya washindwe kuvua au kufuga.Kwa miaka mingi, wanamgambo wamekuwa wakishinikiza serikali kwa kuwateka nyara wafanyakazi wa mafuta na kuanzisha mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa usalama na miundombinu ya mafuta kama mabomba.

Ili kushughulikia suala hili, rais wa zamani, Umaru Musa Yar Adua alizindua mpango wa msamaha wa rais mnamo mwaka 2009, ambao ulimaliza rasmi mtandao wa wanamgambo wa Niger Delta. Lakini vikundi vyenye silaha bado vinaleta changamoto ya usalama katika eneo hilo na maafisa wamekuwa wakionya kuwa wanamgambo wanaanza tena kuchukua udhibiti

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post