Umoja wa Ulaya walaani vitendo vya Urusi dhidi ya waandishi



Umoja wa Ulaya umelaani ukandamizaji wa hivi karibuni unaofanywa na serikali ya Urusi dhidi ya vyombo huru vya habari na mashirika ya kiraia. Msemaji wa waziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amesema kunyamazishwa kwa taasisi huru, sauti muhimu na upinzani ni jambo linalotia wasiwasi kuelekea uchaguzi wa jimbo la Duma mnamo mwezi Septemba. Umoja huo umeitaka Urusi kubadili maamuizi yake na kuacha ukandamizaji huo wa mashirika ya kiraia na vyombo huru vya habari. Taarifa iliyotolewa na msemaji huyo hasa imeutaja uamuzi wa kuiweka Taasisi ya Sheria na Sera ya Umma nchini humo pamoja na waandishi kadhaa wa habari kama mawakala wa kigeni kama jambo lisilo stahili.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post