Jeshi la Urusi lilitangaza wiki jana kwamba limerusha kombora la balestiki na kuharibu ghala kubwa la silaha la chini ya ardhi magharibi mwa Ukraine.
Iwapo itathibitishwa itakuwa mara ya kwanza kwa Urusi kutumia kombora hilo la balistiki la Kinzhal, au Dagger, lililorushwa kutoka angani, uwezekano mkubwa zaidi kwamba lilirushwa na ndege ya kivita ya MiG-31.
Makombora ya hypersonic ni nini?
Rais Vladimir Putin amesisitiza mara kwa mara uwekezaji wa Urusi katika makombora ya hypersonic, ambayo yanaweza kusafiri kwa zaidi ya mara tano ya kasi ya sauti, au Mach 5.
Takwimu ni za kuvutia: kulingana na maafisa wa Urusi Kinzhal inaweza kulenga shabaha hadi kilomita 2,000 (maili 1,240) na inaweza kuruka kwa kasi zaidi ya kilomita 6,000 kwa saa. Lakini je, hilo hulifanya kuwa hatari zaidi kuliko makombora mengine au hata mizinga ambayo inaweza kusababisha vifo na uharibifu vivyo hivyo?
"Siioni kuwa muhimu hivyo," anasema James Acton, mtaalamu wa sera za nyuklia katika Shirika la Carnegie Endowment for International Peace. "Sijui ni faida ngapi Urusi inapata kutokana na kutumia makombora ya hypersonic."
Rais Putin alijigamba mwezi Disemba mwaka jana kwamba Urusi ilikuwa inaongoza duniani kwa makombora ya hypersonic, ambayo ni vigumu kufuatilia kwa sababu yanaweza kubadilisha mwelekeo wakati wa katikati ya ndege.
Urusi ilichapisha video ya kile ilichosema ni shambulizi lake la kombora kwenye ghala la silaha huko Deliatyn, kijiji kilichoko kusini-magharibi mwa Ukraine kilomita 100 pekee kutoka mpaka na Romania.
"Ni ishara ya umahiri. Hata kama itatumika tunapaswa kuiona kama wakati wa pekee kwa sababu Urusi haina idadi kubwa ya makombora haya," Dominika Kunertova wa Kituo cha Mafunzo ya Usalama huko Zurich alisema.
'Haiwezi kubadili mwelekeo wa vita'
Kiongozi wa Urusi alizindua Kinzhal miaka minne iliyopita kama moja ya safu ya silaha "zisizoweza kushindwa" ambazo alisema zingekwepa ulinzi wa adui. Makombora mengine ya hypersonic ni Zirkon na Avangard, ambayo ni ya haraka zaidi na ina safu kubwa zaidi.
Kinzhal inaweza kubeba vichwa vya nyuklia na vile vile vya kawaida na ripoti za hivi karibuni zilisema ndege za MiG-31 zilitumwa Kaliningrad, na kuleta miji mikuu mingi ya Ulaya kufikiwa .
Hakuna dalili kutoka mahali ambapo shambulio kwenye ghala la silaha lilipozinduliwa.
Mwisho wa Twitter ujumbe, 1
"Ni ishara kwa nchi za Magharibi, kwa sababu Putin anakasirishwa na nchi za Magharibi kuthubutu kuhamisha silaha hizi zote [kwa Ukraine]," Bi Kunertova aliambia BBC. "Inatia shaka kuwa ni sahihi sana, kwa hivyo sio jambo la kuweza kubadilisha mwelekeo wa vita'