Halaand ni mchanganyiko wa Cristiano Ronaldo, Zlatan Ibrahimovic na nyota wengine

 

.

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Maelezo ya picha,

'Mchezaji mwenye kila kitu ambacho mshambuliaji angehitaji'

Huenda ilikuwa ni derby ya Manchester lakini kwa Erling Haaland ulikuwa mechi nyengine tu na rekodi nyingine kuvunjwa.

Mabao yake matatu katika kipigo cha 6-3 dhidi ya Manchester United Uwanjani Etihad yalimhakikishia kuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick tatu mfululizo nyumbani kwenye ligi ya Premier League.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amezoea kufunga - na kufunga hat-trick - hata aliweka mkono wake juu ya bega la mwenzake Phil Foden katika mahojiano yao ya baada ya mechi na kusema kwa mzaha kwamba wanaweza kuwa na mpira wa mechi kila mmoja wao. Mshambuliaji huyo wa England pia alifunga mabao matatu dhidi ya United.

Kipa wa zamani wa United na City Peter Schmeichel aliiambia BBC Radio 5 Live unaweza "kuona wachezaji tofauti ndani ya Haaland" na anafanana na "washambuliaji wakuu wote wakiwekwa pamoja".

"Sehemu kubwa ya mshambuliaji mzuri ni uvumilivu. Nilicheza dhidi ya baadhi ya washambuliaji bora na wanapotoweka ndio wakati ambao unapaswa kutahadhari," aliongeza Schmeichel.

"Cristiano Ronaldo, Filippo Inzaghi wa dunia hii - wanatoweka kisha ghafla wanapata nafasi.

"Unapomtazama Haaland, unaona wachezaji tofauti. Hilo goli kama la Zlatan, na Ronaldo yumo pia. Unaona washambuliaji wa viwango vya juu katika moja.

"Ndio maana ni mchezaji hatari sana. Ana uwezo wa kucheza kama washambuliaji wengi wa kiwango cha juu na wote wanachanganywa kwenye mchezaji mmoja."

'Idadi ya magoli inaogofya'

"Ndio, sio mbaya" ndivyo Haaland alivyojibu wakati Sky Sports ilipomuuliza kuhusu uchezaji wake kwenye derby.

"Tulifunga mabao sita. Naweza kusema nini. Kushinda nyumbani, kufunga mabao sita, ni kitu kizuri. Mwishowe, inashangaza. Hakuna la kusema zaidi," aliongeza.

Mara nyingi imekuwa bahati "nzuri" kwa Haaland tangu ajiunge na City, na meneja Pep Guardiola anasema takwimu zake za kufunga "zinatisha".

"Nambari zinajieleza. Amefanya hivi kabla ya kuja hapa. Sio sisi pekee. Kila mara tunajaribu kumsaidia katika mazingira yetu," alisema Guardiola.

"Tunahisi hii  kwamba anaonekana kuwa na njaaya kufunga magoli kila wakati na ni mshindani. Nambari zinatisha."

Hat-trick ya hivi punde zaidi ya Haaland ilimfanya kufikia mabao 17 na kutoa pasi tatu za mabao katika mechi 11 zilizopita.

Tayari amefunga mabao matatu zaidi katika mechi zake nane za kwanza za Premier League kuliko rekodi ya awali ya Mick Quinn, Papiss Cisse na Diego Costa baada ya mechi 10.

Mabao yake tisa katika mechi zake tano za kwanza yalimfanya kuwa mfungaji bora mwezi Agosti wa msimu wowote wa Ligi Kuu.

Fowadi huyo wa Norway pia alikuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika mechi zake nne za kwanza ugenini kwenye Ligi Kuu ya England na ndiye mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kufunga mabao 25 ​​kwenye Ligi ya Mabingwa.

"Sijawahi kufunga hat-trick tatu katika mechi tatu za nyumbani hapo awali. Inashangaza," Haaland aliiambia BBC Radio 5 Live.

"Kujiamini ni kitu kuzuri, imekuwa vizuri kila mara. Baada ya kupoteza kombe la Charity Shield na Liverpool, tumefanya  vizuri. Ilikuwa ni vyema mechi hii ilipojiri na nilijua lazima niwe nimejiandaa.

"Nilihisi siku chache kabla ya Manchester derby kwamba kitu maalum kingetokea na baadhi ya mambo maalum yalifanyika hivyo ni mazuri. Ni mechi kama hizi ninazotaka kucheza."

'Haaland atavunja rekodi iliowekwa na Shearer'

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Je atavunja rekodi ya Shearer ya magoli mengi EPL?

 

Kiwango ambacho Haaland anafunga mabao kilimfanya mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Chris Sutton kusema kwenye BBC Radio 5 Live kwamba "yeye ni kituko".

Pia alimfananisha na mshambulizi mwenzake wa zamani wa Blackburn Rovers, Alan Shearer, ambaye bado anashikilia rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi kwenye Premier League akiwa na mabao 260.

"Ikiwa Haaland atasalia, rekodi ya Shearer itavunjwa. Sina hakika kwamba Harry Kane atafikia hapo. Jamaa huyu anafunga magoli mengi sana .

"Robbie Savage alisema atafunga mabao 51. Huo si uwongo. Ikiwa ataendelea kuwa katika hali nzuri, hilo linawezekana."

Mlinzi wa zamani wa Uingereza Jonathan Woodgate alisema "hajawahi kuona mshambuliaji wa kati mwenye uwezo wa kufunga magoli kama Haaland" na "ana kila kitu".

"Akipata nafasi kwenye lango ni hatari sana. Ana kipaji cha ajabu. Sioni udhaifu kwenye mchezo wake," Woodgate alisema kwenye BBC Radio 5 Live.

"Kama unataka kupigana naye, atapigana nawe. Ukitaka kushinda naye atashinda na wewe .Ana kila kitu ambacho unaweza kutaka katika mshambuliaji wa kati.

"Kama Manchester City wangekuwa na Haaland msimu uliopita, wangeshinda Ligi ya Mabingwa."

'Hatrick Maalum kwa kijana wa nyumbani'

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Phill Foden

Lakini haikuwa Haaland pekee aliyegonga vichwa vya habari Jumapili kwani mhitimu wa chuo kikuu Foden pia alifunga hat-trick yake ya kwanza.

Akiwa na umri wa miaka 22 na siku 127, pia alikua mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kufikisha mabao 50 chini ya usimamizi wa kocha Guardiola, akimpiku Lionel Messi.

"Hat-trick kutoka kwa kijana wa nyumbani ni maalum. Ni nzuri sana kuona. Kupata hat-trick katika derby – ungetaka nini cha no?" beki wa zamani wa City, Micah Richards aliambia Sky Sports.

Woodgate aliongeza: "England inapaswa kujenga timu yao karibu na Foden, yeye ni mzuri sana. Kipaji cha ajabu kama nini."

Shabiki wa maisha yote wa City Foden alisema ilikuwa "ndoto kutimia" kufunga mabao yake ya kwanza dhidi ya Manchester United.

Guardiola aliongeza: "Hamu yake, jinsi anavyokimbia, ndio kitu maalum. Anastahili kucheza kila wakati na kisha ana ubora. Ni mchezaji mdogo anastahili kila kitu.


'Haaland ndiye mshambuliaji mzuri zaidi duniani' - maoni yenu

Adam: Haaland ndiye mshambuliaji bora zaidi duniani hivi sasa. Lewandoski pekee ndiye anayemkaribia.

 

Tim: Wow. Njia pekee ya kumzuia Haaland kufunga ni uhamisho kwenda Chelsea... (Shabiki wa Chelsea).

 

Mahesh: Ni vyema kama Haaland ataendelea kufunga kama hivi, atachoshwa hivi karibuni na kuondoka mapema badala ya kungoja miaka 2.5.

 

Larry: Chakula cha jioni kinapakuliwa. Kevin De Bryune ndio mpishi.

Ruka Twitter ujumbe
Maelezo ya video,Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post